JIFUNZE KILIMO CHA MATONE (DRIP IRRIGATION) WA GHARAMA NDOGO.

Hii ni njia ya kumwagilia mmea kwa kutumia tone(matone) la maji kwa muda husika, ambapo bomba dogo huundwa kwa kuwekewa matundu madogo madogo kwa kuzingatia mmea ulipo kwaajili ya kuupa maji mmea muda wote.
Umwagiliaji huu unaweza kuendeshwa kwa mashine au kwa mkono. Umwagiliaji huu pia unaweza fanyika kwa mazao yaliyo mengi ikiwemo ya mboga mboga, matunda na hata nafaka. Katika maeneo yaliyo mengi umwagiliaji huu wakulima hupendelea kuufanya kwa mazao ya matunda na mboga mboga.

FAIDA ZA UMWAGILIAJI WA MATONE
1.    Matumizi ya maji ni yenye mafanikio.
2.    Mavuno ni ya uhakika.
3.    Mgawanyo wa maji katika mimea ni sawa.
4.    Mmonyoko wa udongo ni mdogo sana.
5.    Hupunguza gharama za wasaidizi shambani.
6.    Huokoa muda. 

CHANGAMOTO ZA UMWAGILIAJI WA MATONE
Kama maji yatakayo tumika katika umwagiliaji yakiwa na chumvi husababisha udongo kuwa na chumvi. Kama miundombinu haitawekwa sawa upotevu wa maji utakuwa mkubwa. 

VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA UMWAGILIAJI WA MATONE 


 1. Topografia Huu ni umwagiliaji wenye mafanikio hakikikisha eneo lako lipo tambarare, hata kama mteremko utawepo uwe mteremko wa wastani, kufanya mgawanyo wa maji kuwa sawa. Pia zingatia sehemu ya kuweka chanzo cha maji inaweza kuwa ni pipa liliwekewa miundo mbinu mizuri miundombinu hiyo kama bomba zilizo sanifiwa vyema kufikia kwenye mmea, pipa au chanzo chochote cha maji hicho kiwekwe sehemu iliyo inuka ili kufanya maji yateremke vizuri kwenye bomba mpaka kwenye mmea.

2. Aina ya udongo ni muhimu sana kujua aina kama ni tifutifu, kichanga au mfinyanzi,hii itakusaidia mkulima kujua uwezo wa aina husika ya udongo wa kuhifadhi maji ardhini.

3. Mgawanyo wa maji. 
Maji ni lazima yawe yenye ubora na maji yawe ya uhakika, kwa kuzingatia hilo pia topografia ya eneo husika ni iwe tambarare au mteremko kiasi Kuruhusu maji kugawanyika vyema kwenye mmea kwa kiwango kile kile na spidi ile ile kwa kila mmea. 


3. Kila zao lina nafasi zake katika upandaji hivyo unavyoweka mfumo wa umwagiliaji hakikisha nafasi unazo weka ziendane na nafasi ya zao husika.


Mfano: JINSI YA KUWEKA MFUMO WA UMWAGILIAJI SHAMBANI 
Vitu vifuatavyo viwepo; vifaa, chanzo cha maji,ukubwa wa shamba. 


VIFAA – katika umwagiliaji huu vifaa vinavyoweza tumika ikiwemo, Chanzo cha maji kinaweza kuwa pipa, hakikisha pipa hili limetobolewa na kupitisha maji mpaka kwenye bomba ambazo zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mmea.

Bomba hizi ziwe zimetobolewa kulingana na nafasi kutoka mmea hadi mmea, na zimewekwa kulingana na mstari kama mistari ipo kumi na bomba ziwe kumi. Sehemu za mfumo huu wa umwagiliaji.
Vali(valvu) Kazi ya hichi chombo ni kuruhusu maji yatoke au yasitoke, ni sawa sawa na koki kama wengine wanavyoita. 

Kichujio ni muhimu sana kwani itasaidia kuchuja maji kuzuia uchafu kama mchanga, nyasi ambazo huenda zikasabibisha matundu yakutolea maji kuziba, hizi chujio ziwekwe kabla ya kufungwa bomba za kupeleka maji kwenye mmea. 


Emmita Haya ndio matundu ambayo yanapeleka maji kwenye mmea, kwa kawaida hutoa maji kwa muda wa saa moja kwa maji lita 4 kwa gallon moja la maji.


Uendeshaji wa mfumo huu wa umwagiliaji
1.    Mfumo huu uendeshwe kwa kuzingatia maji yanafika katika mmea husika kwa kiwango kile kile kwa mimea yote
2.    Hakikisha hakuna upotevu wa maji kama bomba zinavuja hakikisha hazivuji. •Mfumo huu kuwa wenye mafanikio yapaswa ukaguzi wa mara kwa mara ili kuangalia unavyo fanya kazi. 
3.    Hakikisha maji yanafika katika mmea kama inavyotakiwa. Kabla hauja upeleka katika utekelezaji mfumo huu shambani chora kwanza ramani katika katika karatasi halafu nenda ukauweke shambani.


JIFUNZE KILIMO CHA MATONE (DRIP IRRIGATION) WA GHARAMA NDOGO. JIFUNZE KILIMO CHA MATONE (DRIP IRRIGATION) WA GHARAMA NDOGO. Reviewed by BENSON on September 19, 2017 Rating: 5

2 comments

  1. gharama za kuandaa miundombinu hii kwa ekari moja ni kiasi gani kwa wastani

    ReplyDelete
  2. Naomba kujua gharama ya kuweka me undombinu kwa ekari moja

    ReplyDelete