MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UFUGAJI WA VIFARANGA VYA KUKU
Ufugaji
wa kuku imekuwa ni kazi muhimu na inayokubalika katika jamii nyingi. Ni kazi
isiyohitaji gharama kubwa sana, ambayo imekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa
kwa wanaiofanya kibiashara.
Tatizo
ambalo limekuwa sugu na kusababisha hasara kwa wafugaji walio wengi, ni
kutofahamu namna bora ya kuwatunza vifaranga kuanzia siku ya kwanza
wanapoanguliwa hadi kuwa kuku wakubwa. Hali hii imekuwa ikiwasababishia
wafugaji hasara na kuwakatisha tamaa.
Hii
inatokana na wafugaji kuzingatia kuwa na banda na chakula tu, bila kuzingatia
aina nyingine ya matunzo muhimu yanayohitajika kwa ajili ya kuwafanya vifaranga
waishi na kukua wakiwa na afya.
Haya ni
baadhi ya mambo muhimu kuanzia siku ya kwanza ili vifaranga wako wasipate
madhara na hatimaye kufa:
1.
Mara
baada ya kuanguliwa, vifaranga wawekwe sehemu yenye joto kwa wastani
unaohitajika.
2.
Hakikisha
sehemu ya banda ulipowaweka vifaranga ni kavu, na isiyokuwa na vimelea.
3.
Hakikisha
vifaranga wote wanapata chanjo ya mahepe (mareks) siku ya kwanza.
4.
Siku ya saba, vifaranga wachanjwe dhidi ya
ugonjwa wa kideri.
5.
Inapofika
siku ya 14, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa gumboro.
6.
Rudia
chanjo ya kideri katika siku ya ishirini na moja.
7.
Siku ya
ishirini na nane, rudia tena chanjo ya gumboro
8.
Baada ya
wiki nane, hakikisha kuwa vifaranga wako wanapata chanjo ya ndui.
Kwa
kuzingatia mtiririko huo, utakuwa na uhakika kuwa kuku wako ni salama. Watakuwa
bila tatizo, jambo ambalo litakupa uhakika wa kuwa na mazao bora, na hatimaye
kupata faida.
Pamoja na
hayo, hakikisha kuwa unazingatia lishe bora. Hii itasaidia kuwapa kuku afya
njema na kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa.
Kamwe usiwape
kuku vyakula vilivyooza. Hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa kuku na
kusababishia hasara.
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UFUGAJI WA VIFARANGA VYA KUKU
Reviewed by BENSON
on
August 27, 2017
Rating:
No comments