KANUNI BORA ZA UFUGAJI WA SUNGURA
Kabla
hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia
wanyama hawa, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura
wanahitaji uangalizi na hasa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata
maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu.
MABANDA
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda
wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na
mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni
muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa
wanakula watoto wa sungura.
UFUGAJI WA NDANI
1. Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni
vigumu kusafisha.
2 . Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye
ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au
umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa
kuzimeng'enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata
ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3. Ukubwa wa banda usipungue mita 4 x 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa
zaidi ni vizuri.
4. Chini kuwekwe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda
yatokanayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee
kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia
hasa kwa wazazi
5. Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza
kutumia mbao, box gumu au plastiki.
UFUGAJI WA NJE
1. Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine
kama paka, mbwa, mwewe nk
2. Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa
ajili ya sungura kupumzika
3. Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda
mbali
4. Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au
mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu
wakushauri au ng'oa yote)
MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila
siku na vyombo visafishwe kila siku.
CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza
kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama
chakula chenye virutubisho (concentrates).
USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi
kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja
kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia
kujifungua watoto.
MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa
kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili
kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12.
MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa
manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazi
huhitaji kupunguzwa zikikua sana.
UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya
shingo kama paka ukitaka kumbeba.
DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za
wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto,
usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu
kabisa kama nilivyosema mwanzo .
mpaka kufikia hapo hatuna la ziada, tukutane siku ya kesho tukijadili somlo
jijngine kwa undani Zaidi.
KANUNI BORA ZA UFUGAJI WA SUNGURA
Reviewed by BENSON
on
August 26, 2017
Rating:
No comments