YAJUE MADHARA YA KUMFUNGA MBUZI KAMBA SHINGONI.
Kuna baadhi ya wafugaji wamekuwa wana tabia
ya kufunga mbuzi kamba shingoni bila kujua ya kwamba kufanya ni kuns msdhsrs ns
madhara hayo ni ama ambavyo nitaeleza
katika Makala haya ya leo.
Kufunga kamba mbuzi shingoni humsababishia
kudhoofika na kupunguza uzalishaji. Pia, ni rahisi kwa mbuzi aliyefungwa kamba
kushambuliwa na wadudu ambao matokeo yake ni magonjwa ya mara kwa mara, jambo
ambalo litaathiri kipato cha mfugaji.
Mbali na magonjwa,
mbuzi anapofungwa kamba anaweza kuvunjika shingo na kufa, au kuumia vibaya. Inapotokea
akashtuka au kutaka kukimbia anapotokea mnyama kama vile mbwa, mbuzi atajaribu
kukimbia.
Hivyo, kamba
aliyofungwa shingoni kumuumiza. Pia ni rahisi mbuzi aliyefungwa kuathiriwa na hali
ya hewa kama vile jua kali au mvua inaponyesha, mbuzi hawezi kukimbia kujikinga
dhidi ya mvua au jua.
Ni dhahiri kuwa wafugaji wengi wana bidii sana na kuwa na matumaini makubwa
kutokana na kazi zao. Hari ya kuwa na uzalishaji mzuri kutokana na mifugo yao
pia ni dhahiri.
Pamoja na hari
hiyo, wafugaji wengi wamekuwa hawazingatii kanuni bora za ufugaji na utunzaji
wa mifugo yao. Mbuzi wa aina zote wawe wa kisasa au kienyeji wana tabia ya
kupenda uhuru na wanahitaji matunzo mazuri ili kuwa na ufanisi mzuri.
Endapo ni lazima
kuwafuga mbuzi nje ya banda, ni vyema wakatengewa eneo la wazi ambalo litawapa
uhuru wa kutembea huku wakila majani. Ni vizuri mfugaji akajifunza na
kuzingatia njia bora za ufugaji wa mbuzi wa maziwa ili kuepuka kufuga kwa
mazoea na kutopata faida halisi.
YAJUE MADHARA YA KUMFUNGA MBUZI KAMBA SHINGONI.
Reviewed by BENSON
on
August 25, 2017
Rating:
No comments