KILIMO BORA CHA KOROSHO
koroshoo ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae 16 century ndipo
lilipo fika africa katika nchi ya msumbiji na baadae likafika nchini Kenya na
Tanzania.
kwa hapa Tanzania korosho hulimwa na kustawi vizuri katika mikoa ya kusini
Mtwara, lindi, na maeneo kama Mafia, bagamoyo na Rufiji.
Kiwango cha mvua;
korosho ustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua 840mm - 1250 mm
wastani wa mvua kwa mwaka,napia hukua vizuri kwenye maeneo 0- 500 m kutoka usawa
wa bahari.
udongo ufaao kwa kilimo hiki;
korosho ukua vizuri kwenye maeneo yenye PH 5.6 udongo wa
kichanga (sandy) na pia udongo mfinyazi kichanga.
kuandaa shamba.
kama mazao mengine shamba la korosho linatakiwa kusafishwa, kusawazishwa
nakutifuliwa vizuri kwaajili ya kupanda korosho.
nakatika mashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya ngombe ukachanganya na
udongo mapema ili kuongeza rutuba.
kupanda.
Ni muhimu sana kuchagua mbegu bora kwa kua mbegu
utakayo panda ndo itakuonesha kiasi gani utavuna,
11. baada ya kununua mbegu
unachukua maji na chumvi 100g ya chumvi unaweka katika maji kiasi cha lita 5
unakoroga vizuri na unachukua mbegu zako unaweka kwenye maji hayo zile zitakazo
zama ndio mbegu zenye uwezekano mkubwa wa kiota, baada ya hapo unazianika
vizuri hili ziweze kukauka.
kuna aina mbili za upandaji wa korosho ambazo ni:
1.
kupanda moja kwa moja; hii ni njia
mambayo ni risk sana na inaitaji umakini kwa sababu kunauweze3kano mkubwa
wa mbegu kufa. ukitumia njia hii unatakiwa kupanda mbegu tatu 3 katika shimo
moja na baada ya miezi mi 3 - 4 ngoa mimea na bakiza mmoja wenye afya na
muonekano mzuri.
2.
njia ya kitaru; hii ni njia ya pili
na ni nzuri kwa sababu unakua huru kuchagua mche ambao umestawi na ulio na
muonnekano mzuri , unatakiwa kuamishia miche shambani ikiwa na umri wa wiki 6
na zingatia kuchagua mche wenye afya.
Na baadae unatakiwa kupunguza majani urefu wa sm60- 90 kutoka
kwenye ardhi na pia ondoa majani yote ambayo yanaonekana kuadhiliwa na magonjwa
au wadudu na yale yalio kauka.
MAGONJWA NA WADUDU
MAGONJWA
·
Anthracnose
·
powdery mildew
hayo ni magonjwa yanayo athiri thana korosho
WADUDU
·
Cashew stem girdler
·
cashew weevil
·
coconut bug
·
heliotropes bug
·
meal bug
·
trips aphids
namna ya kuzuia wadudu na magonjwa
ili kuzuia maagonjwa na wadudu
unatakiwa
1.
Palilia mapema
2.
Weka shamba katika hali ya usafi
3.
Tumia mbinu ya kuchanganya mazao kwa korosho unaweza kuchanya
pamba au maharage hiyo inasaidia kukimbiza wadudu wengine ambao wanakua
hawapatani na mazao hayo
4.
Tumia pesticide kutibu magonjwa
5.
Tumia insecticide kuuwa wadudu waalibifu.
Kuvuna
1. Korosho ufikia hatua
ya kuzaa matunda pale inapo kua na umri wa miaka 2 1/2 hadi 2. miaka mitatu
2. Pia matunda ukomaa pale inapo kua na miaka 9
hadi 10
3. Uwezekano wa mkoroso kuishi ni miaka 30 hadi
40
4. Lakini pia kuvuna hua kunaanza mwezi october hadi mwezi
december
Mwisho tuangalie matumizi ya korosho
korosho
hutumika kwa matumizi yafutayo;
1. chakula
2. hutumika
kutengeneza rangi
3. Hutumika kama zao la biashara
4. miti yake
hutumkia kama kuni
5. kutengeneza dawa
KILIMO BORA CHA KOROSHO
Reviewed by BENSON
on
July 16, 2017
Rating:
No comments