MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE
Kuku hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo mengine yanatibika kwa dawa na
mengine hayana tiba, ila pia kuku hupewa
chanjo maalumu ambayo huzuia magonjwa hayo. Leo nitawaeleza baadhi ya magonjwa
ambayo hushambulia kuku mara kwa mara na ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa
wafugaji wa kuku.
Tuanze kwa kuangalia magonjwa yaonayohitaji
chanjo ambayo ni
1. GUMBORO
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
Dalili za ugonjwa
-Kuku kuzubaa na kulundikana, pamoja na kusinzia
-Kuku kuharisha
-Kuwa na vifo vingi kwa kuku
Tiba.
Ugonjwa huu
hauna tiba,,Kuku wakipewa Dawa za oxytetracycline hupunguza vifo.
Kinga
wakinge
kuku wapo kwa kuwapa chanjo ya gumboro (Gumboro vaccine)
2. MAHEPE
(Marecks)
Ugonjwa huu husababishwa na
virusi
Dalili za ugonjwa.
-Kuku hupata ulemavu na vifo vya mara kwa mara.
Tiba za ugonjwa huu.
Ugonjwa huu
hauna tiba
Kinga za ugonjwa huu.
Chanjo hutolewa
kwa vifaranga wenye umri wa siku moja,vifaranga hupewa chanjo ya mahepe (Marecks
vaccine)
3. NDUI YA KUKU (Fowl Pox)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
Dalili za ugonjwa huu ni;
-Kuku hupatwa na vidonda kichwani.
-Kuku hupata uvimbe mweupe kwenye mdomo na kushindwa kula.
Tiba za ugonjwa ndui
Ugonjwa huu hauna tiba.
Kinga za ugonjwa huu.
Chanja kuku wako
wa siku 60-90 kwa chanjo ya Ndui ya kuku (Fowl pox vaccine).
4. MDONDO
Ugonjwa huu husababishwa na virusi
Dalili za ugonjwa wa mdodndo
-Ugonjwa huu hutokea kwa ghafla na kuenea kwa haraka
-Vifo vya kuku huwa vingi
-kuku hupumua kwa shida
-Kuku hupooza na kulemaa miguu
-Kuku hupinda shingo yake
-Kuku hupunguza kutaga mayai
-kuku huarisha
-Kuku Kuzunguka zunguka na kutembea kinyume nyume.
Tiba za ugonjwa za mdondo
Hauna tiba
Kinga za ugonjwa wa mdondo.
Chanja vifaranga wako na kuku wako kwa chanjo ya Mdondo (New castle vaccine) na
urudie chanjo hii kila baada ya miezi mitatu.
Somo litaendelea siku ya kesho……..
MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE
Reviewed by BENSON
on
July 17, 2017
Rating:
No comments