MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA WAKATI WA UVUNAJI WA VIAZI VITAMU.

Related image
Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Aina nyingine ya vyakula vya aina ya mizizi ni kama mihogo. vile  Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Zao la viazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini.

Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, iringa, Morogoro, Kagera, Arusha na Ruvuma na maeneo mengineyo.

Mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa uvanaji wa viazi vitamu;

Viazi vitamu huwa tayari kuvunwa miezi mitatu hadi minne tangu kupanda kutegemea hali ya hewa. Viazi vinaweza kuvunwa kidogo kidogo kwa kutumia mikono, vijiti, jembe, au rato kadri vinavyohitajika. Aidha inashauriwa viazi visiachwe ardhini muda mrefu bila kuvunwa kwani vitakomaa sana na kuwa na nyuzi, na hivyo kuharibu ubora wake.

Pia kuacha viazi muda mrefu hukaribisha mashambulizi ya wadudu kama fukusi  ambavyo husababisha kuoza. Kwa maeneo makubwa zaidi, inashauriwa kutumia mashine ya kukokotwa na ng’ombe. Uvunaji ufanywe kwa uangalifu ili kuhakikisha viazi visikatwekatwe wala kuchubuliwa wakati wa kuvuna.

Mavuno ya viazi hutofautiana kulingana na aina, hali ya hewa, na udongo. Mavuno ya viazi yanakadiriwa kufikia tani 20 kwa hekta kama endapo mkulima atazingatia kilimo bora cha viazi vitam
MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA WAKATI WA UVUNAJI WA VIAZI VITAMU. MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA WAKATI WA UVUNAJI WA VIAZI VITAMU. Reviewed by BENSON on June 09, 2018 Rating: 5

No comments