UFUGAJI BORA WA BATA BUKINI
Bata Bukini ni ndege ambao asili yao
ni India na Japan. Hii ni jamii ya ndege wafugwao lakini tofauti kubwa ya bata
wa kawaida wao wana asili ya usafi, hivyo hawapendi uchafu na kamwe hawali
mizoga.
Tofauti na ndege wengine au bata
wengine wa kawaida, mfugaji wa bata bukini anaweza kupata kipato kikubwa kwa
haraka na kwa gharama ndogo ukilinganisha na bata wengine.
Kuna aina mbili ya bata bukini ambao ni weupe na wenye mchanganyiko
wa rangi. Hali kadhalika hutofautiana katika utagaji wa mayai.
Chakula
Ndege hawa wanakula chakula kama wanacholishwa kuku, wanapendelea kula majani
jamii ya mikunde kwa 50% na hawahitaji chakula kingi. Vifaranga ni lazima
wapatiwe lishe kamili hasa protini kwa wingi ili waweze kujenga mwili, kukua
vizuri na kuwa na afya nzuri.
Kwa maana hiyo, vifaranga wanahitajika kupata walau 20% ya
protini kwa wiki mbili za awali na baada ya hapo waweza kupunguza hadi 15%
kulingana na kukua kwao hadi wanapokuwa wanaelekea kukomaa.
Kama ambavyo mfugaji anaweza kutengeneza chakula kwa ajili
ya mifugo wengine, pia anaweza kutengeneza cha bata bukini kama ifuatavyo:
Mahitaji
1. Mahindi kilo 10 ( hakikisha hayana dawa)
2. Chokaa kilo 5 (ya kulishia mifugo)
3. Dagaa kilo 10 (wanaotumika kulishia kuku)
4. Mashudu kilo 20.
Utengenezaji na Uhifadhi
Baada ya kupima vyakula hivi kwa usahihi chukua pipa, changanya vizuri kisha
walishe bata kulingana na wingi wao na uhakikishe wanapata chakula cha kutosha.Vipimo
hivi hutegemea wingi wa bata unaowafuga lakini hakikisha uwiano huo
unazingatiwa. Baada ya kutengeneza chakula unaweza kuhifadhi katika mifuko na
kuweka katika eneo lisilokuwa na unyevu.
Kuatamia
Jinsi ilivyotofauti katika idadi ya utagaji wa mayai hivyo ndivyo uwezo wa
kuatamia pia ulivyo. Bata Bukini weupe huatamia mayai 6 na wale wa rangi
huatamia mayai 12
Ndege hawa huatamia kwa siku 29, huangua vifaranga kwa siku 3 na mara nyingi
hutotoa mayai yote, si rahisi mayai kubaki bila kutotolewa au kuharibika.
Namna ya kutunza vifaranga
Mara tu vifaranga wanapoanguliwa, wachukue na kuwatenga na mama yao kisha
waweke katika banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya umeme
kama una uwezo ili kuwatengenezea joto.
Pia, waweza kuzungushia banda lao kitu kizito kama blanketi ili kuwakinga na
baridi au upepo.
Banda
Bata Bukini wanahitaji nafasi ya kutosha hivyo andaa banda kulingana na wingi
wa bata unaotarajia kufuga.
Hakikisha banda limesakafiwa au banda la udongo
lisilotuamisha maji au unaweza kuweka mbao au mabanzi kisha unaweka maranda ili
kuwakinga na baridi.
Maji
Ni lazima bata wapatiwe maji ya kunywa kila siku na
hakikisha banda halikosi maji wakati wote. Safisha chombo cha maji na
kubadilisha maji kila siku.
Ndege hawa wanahitaji maji ya kunywa ya kutosha kama ilivyo kwa kuku. Hakikisha
maji yako kwenye chombo ambacho hayatamwagika , kwani kumwagika kunaweza
kusababisha kuibuka kwa magonjwa. Bata Bukini hawapendi uchafu. Hivyo maji yawe
mahali ambapo hayatachafuka.
Magonjwa
Ni mara chache sana bata bukini kushambuliwa na magonjwa kama watawekwa katika
hali ya usafi. Magonjwa yanayoweza kuwasumbua ni mafua na wakati mwingine
kuharisha.
Tiba za asili
Unaweza kutibu bata bukini kwa njia za asili. Tumia mwarobaini, vitunguu (maji
na saumu).
1. Mwarobaini
Unaweza kutumia dawa
hii kutibu mafua kwa bata bukini wakubwa au vifaranga.
Maandalizi
Chukua kiasi kidogo cha mwarobaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua
maji ya mwarobaini, kisha changanya na maji uliyo andaa kuwanywesha vifaranga.
2. Kitunguu Saumu na Kitunguu Maji:
Dawa hii hutumika kukinga na kutibu bata bukini wanaoharisha.
Maandalizi
Unachukua kitunguu saumu au maji na kuondoa maganda ya nje
kisha safisha na kukata vipande vidogovidogo na kuwawekea kama chakula.Unaweza
kuwapatia kila siku hadi watakapopona.
3. Majani: Bata Bukini chakula chao kikubwa ni majani. Majani yana
vitamini A, hivyo hakikisha unawapatia ya kutosha. Wapatie majani jamii ya
mikunde.
Kutaga
Bata Bukini huanza kutaga baada ya miezi saba na hutaga mara tatu kwa mwaka.
Isipokuwa, utagaji wa bata bukini weupe na wa rangi hutofautiana katika idadi
ya mayai, Bata Bukini weupe hutaga mayai sita tu lakini wale wa mchanganyiko wa rangi
hutaga mayai kumi na mbili (mara mbili ya weupe)
UFUGAJI BORA WA BATA BUKINI
Reviewed by BENSON
on
August 04, 2017
Rating:
Nitawapataje hawa bata,wanauzwa wapi na bei gani, mayai yake yanapatikana je? na ni beigani?Je mayai yake unaweza kuyaweka au kuangulisha kwa Incubeter?
ReplyDeleteNaomba nijulishe kwa namba 0766242491Jinsi ya kuwapata bata Bukini
ReplyDeleteNiko Dar. Nitafute +255 754364248
DeleteAnaehitaji nichek kwa namb hiz +255(0)692434375
ReplyDeleteWanaanza kutaga baada ya muda gani?
ReplyDeleteWanaanza kutaga baada ya muda gani na wanataga Mara ngapi kwa mwaka?
ReplyDeleteNahitaji mayai ya bikini
ReplyDeleteVifaranga vinapatikanaje kama mtu anahitaji na ni wapi vinapatikanaje
ReplyDeleteNahitaji kuwasiliana na nyinyi zaidi
ReplyDeleteNitapata wapi mbegu hii?
ReplyDeleteNitafute +255 754364248
DeleteAnayehitaji Bata Bukini Piga Namba hii 0713542400
ReplyDeleteAnayehitaji Bata Bukini Piga Namba hii 0655560000
ReplyDeleteSucceeded
ReplyDeleteBata bukini weupe na wale wa rangi wanaweza kuzaliana au ni kila rangi inajitegemea?
ReplyDeleteVipi kuhusu maji ya kuogelea. Naona wasipoogelea hata kujamiiana kunakuwa na shida. Unatushaurije
ReplyDeleteVifaranga tshs ngapi
ReplyDelete👌👍
ReplyDelete