UMUHIMU WA KUTENGENEZA VIOTA VYA KUTAGIA MAYAI

Related image
Viota ni mahali ambapo kuku hutaga mayai, kuhatamia na kuangua vifaranga. Hii inamaanisha kuwa viota ni sehemu muhimu sana ya kuzingatia ili kuweza kupata mayai mengi yaliyo salama pamoja na vifaranga.
Kuku anapotagia porini, mayai huliwa na wanyama kama vile nyoka na wengineo. Kuku pia anaweza kudhuriwa na wanyama hao na wakati mwingine kuibwa. 
• Kwa kuwa na viota vya kutosha itapunguza usumbufu wa kuingia kukusanya mayai kwa mfugaji.
• Njia mojawapo ya kuzuia kuku kula mayai.
• Upotevu wa kuku na mayai utapungua.
• Utapata mayai bora kwa ajili ya kutotolesha.
• Kupunguza mayai kupasuka, pia mayai kuwa safi.
• Kuku kuwa huru wakati wa kutaga au kuhatamia.


UMUHIMU WA KUTENGENEZA VIOTA VYA KUTAGIA MAYAI UMUHIMU WA KUTENGENEZA VIOTA VYA KUTAGIA MAYAI Reviewed by BENSON on January 08, 2018 Rating: 5

No comments