JINSI YA KUJENGA BANDA BORA LA KUKU WA KIENYEJI

Banda bora ni muhimu ili ufugaji wa kuku wa kienyeji uweze kuleta manufaa kwa mfugaji. Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali kama wezi, wanyama wakali, jua kali au mvua.

1.SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU
Liwe na kuta, paa na sakafu imara. kuta na sakafu zisiwe na nyufa Liwe na sehemu ya kuku kutagia, kuatamia na sehemu ya kulea vifaranga. Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala. Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku Liwe na uwezo wa kuingiza mwanga na hewa ya kutosha. Liwe na nafasi inayoruhusu mtu kuingia na kufanya usafi.

2.SEHEMU INAYOFAA KUJENGA BANDA LA KUKU.
Isiyokuwa na mteremko mkali. Isiyoruhusu maji kutuama. Iwe sehemu inayoruhusu hewa na mwanga wa kutosha. Ikiwezekana iwe sehemu yenye kivuli.

3.AINA ZA MABANDA YA KUKU.
Uchaguzi wa aina ya banda la kuku hutegemea mazingira. Kuku wanaofugwa kwenye mazingira ya joto wanahitaji banda lenye ukuta mfupi na sehemu kubwa ya uwazi wenye wavu hadi kufikia kwenye paa kulinganisha na sehemu zenye baridi ambapo,banda linahitaji kuwa na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu,iliyo na uwazi wenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.vilevile eneo lenye matatizo kama ya majimaji au wanyama wanaoshambulia kuku inabidi kujenga aina ya banda lenye sakafu iliyonyanyuliwa juu.

4.VIFAA VINAVYOTAKIWA KATIKA UJENZI WA BANDA.
Vifaa vya kujengea banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo husika.Vifaa hivyo vimepangwa katika makundi yafuatayo:
1. Vifaa vya kujengea sakafu Sakafu la banda la kuku linaweza kujengwa kwa kutumia,saruji,udongo,mbao,mianzi au fito.
2. Vifaa vya kujengea kuta kuta zinaweza kujengwa kwa kutumia , fito,udongo,matofali,mawe,mabati,mianzi,wavu,mabanzi au mbao.
3. Vifaa vya kujengea paa. Paa la banda la kuku linaweza kuezekwa kwa kutumia nyasi, makuti, bati, migomba na vigae kulingana na uwezo wako.
4. Vifaa vya kujengea wigo Wigo unaweza kujengwa kwa kutumia mbao,mianzi,matete,wavu,matofali,miti, au fito,mabanzi au mabati.

UKUBWA WA BANDA LA KUKU KULINGANA NA IDADI YA KUKU
Ukubwa wa banda la kuku unategemea na idadi ya kuku na aina ya kundi la kuku.Kuku wanaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali kutegemea umri wao na madhumuni ya uzalishaji.

BANDA LA VIFARANGA WADOGO WA KUKU NA UKUBWA WAKE 
(UKUBWA WA BANDA LA VIFARANGA WADOGO)
Vifaranga wa siku moja hadi wiki nane Kundi hili la kuku wadogo hivyo wanahitaji eneo dogo la mita mraba 0.075 kkwa kuku mmoja,hivyo vifaranga 100 wanahitaji eneo la mita mraba saba na nusu (urefu wa mita 2.5 X na upana wa mita 3).

BANDA LA VIFARANGA WAKUBWA
banda la vifaranga wa kuku wa wiki tisa hadi 20. Kuku mmoja wa umri huu anahitaji mita za mraba 0.15,hivyo kuku 100 wanahitaji mita za mraba 15 (urefu wa mita 5 X na upana wa mita 

•BANDA LA KUKU WAKUBWA
Ili linajumlisha kuku wa wiki 21 na zaidi.Mara nyingi kundi hili ni la kuku waliopevuka (majogoo na majike wanaotaga) ambalo kuku mmoja huitaji mita mraba 0.2  hivyo kuku 100 huitaji mita za mraba 20 (urefu wa mita 5 X upana wa mita 4).

UKUBWA WA WIGO
Mabanda yanayozungushiwa wigo kama ilivyo katika mfumo wa nusu huria ,kuku mmoja huhitaji eneo lenye ukubwa wa mita mraba 10 hivyo kuku 100 huhitaji eneo la mita za maraba 1000 (urefu wa mita 50 X upana wa mita 20). Kumbuka unaweza kupunguza vipimo lakini uwe mwangalifu na mahitaji ya kuku kwani kadri watakavyosongamana katika eneo dogo ndivyo watakavyohitaji uangalizi mkubwa zaid


JINSI YA KUJENGA BANDA BORA LA KUKU WA KIENYEJI JINSI YA KUJENGA BANDA BORA LA KUKU WA KIENYEJI Reviewed by BENSON on August 20, 2017 Rating: 5

7 comments

  1. Ipo pw ndg but banda hilo linacost shiling ngap

    ReplyDelete
  2. Halafu banda LA kuku wa kienyeji wanahitajika kufanya usafi kila baada ya muda gani au ni kila siku?

    ReplyDelete
  3. Makadirio ya fedha kwaajili ya kujenga banda no bei gani pia kuhusu swala LA USAF/ kusafisha banda n baada ya mda gan?

    ReplyDelete
  4. natamani niwe na kuku wengi nifanyeje na niwe na ufugaji bora

    ReplyDelete