MAMBO MUHIMU ZA KUZINAGATIA WAKATI WA UPANADAJI WA STRAWBERRY

Image result for STRAWBERRY
Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata soko la uhakika, bila vipingamizi, inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya kuzalishia mazao (green house). Katika kuzalisha strawberry baada ya kujenga green house andaa mabomba ya plastiki ambayo yatawezesha kutoboa matundu kwa urahisi Matundu katika bomba hilo yawe na umbali wa inchi 1.
1.    Ni vyema matundu hayo yakawa zigzag, ili kuruhusu mimea utakayopanda kukua vizuri bila kuwekeana kivuli.
2.   Tandika karatasi la nailoni sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea kurudi kwenye bwawa au sehemu ya kuhifadhia.
3.     Ning’iniza mabomba hayo kwa kutumia waya.
4.     Jaza kokote, yenye mapande makubwa kiasi.
5.    Panda miche kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe na kokoto zinazoshikilia mmea. Kumwagilia Mimea ya strawberry inahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana. Hii inamaanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili.
6.    Unapaswa kumwagilia mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii itawezesha mimea yote kupata maji ya kutosha. Endapo strawberry haitapata maji ya kutosha, uzalishaji wake pia utakuwa ni hafifu sana, kwani maua ya Strawberry inapooteshwa kwenye greenhouse hutoa mavuno mengi na yenye ubora yatachanua ipasavyo na hata matunda kukomaa inakuwa ni shida.
MAMBO MUHIMU ZA KUZINAGATIA WAKATI WA UPANADAJI WA STRAWBERRY MAMBO MUHIMU ZA KUZINAGATIA WAKATI WA UPANADAJI WA STRAWBERRY Reviewed by BENSON on June 10, 2018 Rating: 5

No comments