MADHARA YA KUTOKUPALILIA SHAMBA KWA WAKATI
Asante
ndugu msomaji kwa kua nasi siku zote, na napenda kuanza kukupaelimu kwa mara ya
kwanza ndani ya mwaka huu.
na
leo nitaelezea kuhusiana na hasara za kutokupalilia mapema na faidia za
kupalilia shamba lako mapema.
Wakulima
wengi sana wamekua wakilichukulia swala la kupalilia kama ni swala la hiali tu,
lakini ukweli ni kwamba wewe kama mkulima na unalengo la kupata mazao mengi
yenye ubora swala la kupalilia kwa wakati ni swala la muhimu sana hivyo ni
muhimu kulizingatia.
KUPALILIA-Kwa tafsiri rahisi
kupalilia ni ilie hali ya kuondoa memea au majani ya saio itajika(magugu)
shambani. kwa kitaalamu kitendo hiki kinaitwa (WEEDING).
Mkulia
unaweza kuchagua njia sahihi ya kupalilia kulingana na uwezo, ukubwa wa shamba
na aina ya mimea uliyo panda, kuna njia tofauti tofauti ya kupalilia kama
zifuatazo
- kwa
kutumia jembe la mkono
- kwa
kutumia madawa(herbicides)
- kwa
kutumia jembe la ng'ombe
- kwa
kung'olea
usisite
kuendelea kujifunza mengi zaidi kwa kujiunga moja kwa moja na blogi hii HAPA
MAGUGU-
magugu ni mmea wowote ule unao ota sehemu ambayo haiitajiki mfano kama shamba
lako unapanda mpungu na ndani ya shamba ikawepo memea ya mahindi hivyo kwa
wakati hua mahindi ni magugu na yanatakiwa kuondolewa shambani
pia
kuna aina tofauti tofauti ya magugu kwa wakati mwingine nitakuletea somo la
magugu na aina tofauti tofati ya magug, kwa somo letu la leo nitakuonesha
kuhusiana na hasara za kutokupalilia kwa wakati muafaka.
MADHALA
YANAYO YANAYO TOKANA NA UWEPO WA MAGUGU SHAMBANI
Kama
nilivo elezea mwanza kua kuna hasara ya kutokupalilia kwa wakati, hivyo hapa
nitaelezea hasara zinazo wezwa kulutwa na uwepo wa magugu shambani.
- magonjwa
- uwepo
wa wadudu waharibifu
- kugombea
kwa virutubisho
- kugombea
kwa mwanga
- kufa
kwa mimea
- kupunguza
ubora wa mazao
- na
madhara makuu ni kukosa kwa mazao stahiki yaani kupata kidogo
ukilinganisha na jinsi ulivo takiwa kupata.
NOTE; Hivyo ni muhimu sana
kuzingatia kupalilia mapema na unaweza kupalilia mara mbili au zaidi kulingana
na aina ya mmea au zao.
MADHARA YA KUTOKUPALILIA SHAMBA KWA WAKATI
Reviewed by BENSON
on
January 20, 2018
Rating:
No comments