FAIDA YA KULIMA BUSTANI YA MBOGA MBOGA NYUMBANI KWAKO.
Katika
maisha ya familia ni lazima kujituma katika mambo yanayowezekana angalau
kupunguza gharama za maisha yanayoikabili familia. Leo tumeona ni vyema
tukafahamu mambo muhimu tunayoyapuuza, lakini yanaweza kusaidia kupunguza ukali
wa maisha.
Kilimo cha mboga mboga ndani ya familia ni hatua pekee ya kupunguza ukali wa
maisha na kuepuka gharama zisizo za msingi ndani ya familia. Hapa nazunguzia
kwa wale wenye maeneo binafsi na wanaishi mjini au hata vijijini, tumia eneo
ulilonalo kulima hata matuta mawili tu ya mboga mboga; kwamfano nyanya, sukuma
wiki, mchicha na kadhalika.
Tumia nafasi ulionayo hata kama ni kutumia makopo kama maua, panga miche yako
ya nyanya na sukuma wiki au mchicha, ili kuokoa pesa yako kwenda sokoni kila
siku. Kuna baadhi ya mboga mboga huchukuwa siku chache kuota na kukua; kwamfano
mchicha huchukuwa siku chache tayari unavunwa.
Kuwa na bustani ndogo ya mboga mboga nyumbani haikushushi hadhi hata kama wewe
ni tajiri, unaweza kumpa maelekezo msaidizi wako pale nyumbani akapanda hata
matuta mawili tuu ya karoti au nyanya, endapo wewe uko bize.
Bustani ya mboga mboga katika ngazi ya familia sio tuu inasaidia kupunguza
matumizi bari inakupatia uzoefu wa kujituma katika kazi. Kwamfano wenzetu wa
majuu hutenga muda wao wa jioni na asubuhi sana kufanya kitu katika bustani zao
aidha za maua au mboga mboga. Kama bado hukujua utamu wa bustani, basi anza
leo.
FAIDA YA KULIMA BUSTANI YA MBOGA MBOGA NYUMBANI KWAKO.
Reviewed by BENSON
on
January 22, 2018
Rating:
No comments