YAJUE MAGONJWA HAYA AMBAYO HUSHAMBULIA VITUNGUU KWA KIWANGO KIKUBWA.
Mara nyingi unapojikita katika kilimo cha vitunguu yapo mambo
ambayo kiukweli huwa hayakwepi miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na magonjwa
ambayo hushambulia vitunguu
Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako.
Pia magonjwa kama kutu ya majani husababisha na
unyevu mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea
kumwagiliwa jioni au usiku, kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili
kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu
vya kuulia fangasi wa mimea
Lakini inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka
mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza
kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo.
YAJUE MAGONJWA HAYA AMBAYO HUSHAMBULIA VITUNGUU KWA KIWANGO KIKUBWA.
Reviewed by BENSON
on
November 09, 2017
Rating:
No comments