UJUE UGONJWA (FMD) AMBAO HUATHIRI WANYAMA KWA KIWANGO KIKUBWA.
FMD uu ni
ugonjwa unaowashika ng’ombe, kondoo, mbuzi, pamoja na wanyama wa porini kama
mbogo, swala na wakati mwingine tembo. Ng’ombe anapopatwa na ugonjwa wa
miguu na midomo huchechemea na asipotibiwa kwa haraka hushindwa kusimama na
kula hatimae hudhoofika na hata kufa.
Ugonjwa
wa miguu na midomo husambaa haraka kwenye kundi ukiua ndama na kusababisha
wanyama kupoteza uzito na uzalishaji wa wengine kupungua.
Namna
unavyoambukizwa
Ugonjwa
huu unaambukiza kwa kugusana kwa mnyama mmoja na mwingine. Unaweza vile vile
kusambazwa na upepo kwenye umbali hata wa kilometa 250. Pamoja na kusambaa kwa
umbali huo, ni nadra kwa binadamu kupata ugonjwa huu.
Kwa
muongo mmoja uliopita, wastani ugonjwa huu ulikuwa unashambulia kundi mara moja
kwa mwaka. Kwa sasa, katika sehemu nyingi za Afrika Mashariki, ugonjwa unatokea
mara tatu kwa mwaka. Aidha, jinsi hali ya hewa inavyokuwa ya joto la juu,
yanatokea matabaka mapya ya vimelea visababishavyo ugonjwa huu.
Dalili
• Kuwepo
mifugo yenye dalili za mafua, na kuchechemea kwa wakati huo huo.
• Ndama
kufa kwa ghafla kutokana na ugonjwa wa moyo.
Tahadhari
Ugonjwa
wa miguu na midomo una madhara makubwa kiuchumi hasa ukizingatia kuwa,
uzalishaji wa maziwa wa ng’ombe waweza kupungua kwa asilimia 75 kwa maisha yake
yote.
Mbali na
hayo, ng’ombe badala ya kuzaa kila mwaka au kwa vipindi kama hivyo, anaweza
kuzaa kila baada ya miaka miwili au mitatu.
Namna ya
kuzuia
Chanjo
kwa ajili ya ugonjwa huu husaidia kuzuia isipokuwa gharama yake ni kubwa kwani
chanjo hizo zinanunuliwa kutoka nchi za nje na lazima iwe ya kufanyakazi dhidi
ya aina nyingi za vimelea. Hata hivyo, jamii inaweza kupanga, na kununua chanjo
kwa kushirikiana.
Ugonjwa
wa miguu na midomo ni tishio, hasa katika maeneo ambapo mifugo inatumia ardhi
ambayo pia inatumiwa na mbogo na nyumbu. Ni vyema kwa wale wanaoishi katika
maeneo hayo kuhakikisha kuwa ardhi wanayotumia kulishia mifugo yao si ile
inayotumiwa na wanyama pori.
Ugonjwa
wa nyumbu (Malignant Catarrhal Fever -MCF)
Ugonjwa
wa Nyumbu ni ugonjwa ambao husababishwa na virusi aina mbili kwa ng’ombe. Aina
ya kwanza husambazwa na kondoo na mbuzi wakati aina nyingine husambazwa na
nyumbu na pofu.
Aina ya
pili ni tatizo kubwa hasa wakati na mahali ambapo nyumbu wanazalia. Virusi
vinawaachia watoto wa nyumbu wanapotimiza miezi mitatu baada ya kuzaliwa.
Kwa karne
nyingi, ugonjwa wa nyumbu ulikuwa hauwaletei wafugaji madhara makubwa kwa
sababu walikuwa wanahamisha mifugo yao kwenda sehemu nyinginezo kila mwaka katika
kipindi ambacho nyumbu wanazaliana.
Mpango
huu wa kimila wa matumizi ya ardhi umesambaratika, ijapokuwa ni katika miongo
michache iliyopita, kufuatia kuongezeka kwa mahitaji ya kutumia ardhi
(mashindano) na hivyo ng’ombe na nyumbu kulazimika kupata malisho katika eneo
moja hata katika vipindi nyeti ambapo nyumbu wanazaa. Bila kuchukua hatua za
tahadhari, ng’ombe na nyumbu wataendelea kula katika eneo moja na hivyo
uwezakano wa ugonjwa wa nyumbu kuongezeka pia ni mkubwa.
Dalili
Macho ya
ng’ombe yanakosa uwezo wa kupitisha mwanga. Baada ya hapo mnyama anapofuka na
kufa.
Kuzuia na
kudhibiti
Hadi
kufikia sasa, hakuna chanjo wala tiba ya ugonjwa huu isipokuwa suala la
udhibiti unawezekana kwa kupitia matumizi mazuri ya ardhi. Mipango ya matumizi
ya ardhi inabidi izingatie mahitaji ya wafugaji na uhamaji wa nyumbu na mazalia
yao. Mipango inaweza kuweka eneo tofauti la malisho ya mifugo kwenye majira ya
nyumbu kuzaa, ambayo kwa wastani yanaanza mwishoni mwa mwezi Februari hadi Mei.
UJUE UGONJWA (FMD) AMBAO HUATHIRI WANYAMA KWA KIWANGO KIKUBWA.
Reviewed by BENSON
on
November 08, 2017
Rating:
No comments