YAJUE MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE.

Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa yafuatayo:

Ugonjwa wa Newcastle(kideli)
Ugonjwa huu ndio huathiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate.

Dalili
• Kuhalisha choo cha kijani na njano
• Kukohoa na kupumua kwa shida
• Kuficha kichwa katikati ya miguu
• Kukosa hamu ya kula na kunywa
• Kutoa kamasi na machozi
• Kupooza na kuzungusha kichwa na kutembea kinyumenyume
• Idadi kubwa ya vifo hadi 90%

Kinga
•Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
• Epuka kuingiza kuku wageni
• Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
• Zingatia usafi wa mazingira

Minyoo
Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutibu minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya nipiperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur audawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu

Wadudu kama viroboto,Utitiri na chawa
Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri husababisha harara ya ngozi, kuku walio athiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali hii hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa matundu) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku150). Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.
Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.
• Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia
• Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa
• Nyunyiza dawa kwenye viota
• Weka maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku
• Fuata kanuni za chanjo
• Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku wazima

Magonjwa ya mapafu
Magonjwa ya mapafu huathiri njia inayopitisha hewa na kuambatana mate na sauti kama ya kikohozi. Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji wake pia hutokea polepole na vifo sio kwa wingi. Hata hivyo, Tatizo hili laweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga walipoanguliwa hadi pale walipouzwa.


Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu. Kiasi cha milligram 35 ya tylosin hutosha kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii hukomesha madhara yanayotokanana magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakatimmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo. Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya gramu 4.

Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili vya maji), kiasi hiki chaweza kutolewa kwa vitone kwa kila kuku.
Ndui ya kuku/ fowl pox
Ndui huathiri sana vifaranga wanaokua hasa wakati wa mvua, Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu. Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hauna tiba.


Dalili
• Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana kama kishungi,usoni na chini ya mdomo
• Kukosa hamu ya kula
• Vifo vingi

Kinga
• Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
• Epuka kuingiza kuku wageni
• Zingatia usafi wa mazingira.


Ukosefu wa vitamin A
Huathiri zaidi kuku wadogo wanaokua, macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowa maji, kuku wenye ukosefu wa vitamin A hawaponi na hatimaye hufa.Mara kwa mara ugonjwa hujitokeza wakati wa kiangazi,kinga ni kuwapa kuku mchicha au majani mabichi mara kwa mara pia wape kuku wote dawa ya vitamin za kuku zinazouzwa maduka ya mifugo ili kuzuia kujitokeza kwa ugonjwa huu.
Mafua ya kuku/infectious coryza
Hutokana na bakteria na hushambulia hasa kuku wakubwa


Dalili
• Kuvimba uso
• Kamasi zilizochanganyikana na usaha unaonuka
• Macho huvimba na kutoa machozi na pengine upofu
• Hukosa hamu ya kula
• Mbawa huchafuka na kutoa harufu mbaya


Tiba
Dawa za Antibiotic, sulfa na vitamin

Kuhalisha damu/coccidiosis
Husababishwa na vijidudu vya Protozoa


Dalili
• Kuharisha damu
• Manyoya husimama
• Hulala na kukosa hamu ya kula

Homa ya matumbo/fowl typhoid
• Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
• Kuku hukosa hamu ya kula
• Kuku hukonda
• Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
• Kinyesi hushikamana na manyoya


Tiba
Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini 
Kinga
• Usafi
• Fukia mizoga
• Usiingize kuku wageni
• Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6



YAJUE MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE. YAJUE MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE. Reviewed by BENSON on October 02, 2017 Rating: 5

3 comments