KANUNI ZA KILIMO BORA CHA VITUNGUU.
Vitunguu
ni moja ya zao la bustani linalopendwa na kutumiwa kwa wingi sana si
hapa nchini tu bali duniani kote kwa ujumla. Linachukua nafasi ya pili
baada ya nyanya. Kitunguu kinatumika katika kachumbari, kama kiungo
kwenye kitoweo kama vile Samaki, nyama, mboga za mahani n.k. Majani ya
vitunguu hutumika kama mboga. Vitnguu pia hutumika kuandalia supu.
Vitunguu hustawi maeneo yasiyo na mvua
nyingi sana, yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na maeneo yasiyo na
joto kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaa kwa vitunguu.
Vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo
wenye rutuba ya kutosha, unaoruhusu mizizi kupenya na unaohifadhi unyevu
kama vile udongo wa nusu mfinyanzi nusu tifutifu.
UPANDAJI WA MBEGU ZA VITUNGUU KWENYE KITALU.
Hapa kwetu Tanzania upandaji huanza
mwezi March hadi Mei kutegemea na msimu wa kilimo ulivyo. Hivyo kilimo
hiki huanza mara baada ya mvua kubwa za masika kumalizika. Kipindi cha
kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri wa vitunguu.
Mbegu za vitunguu huoteshwa mapema
katika kitalu. Mbegu zinaweza kutawanywa au kupandwa kwa mistari katika
tuta la kitalu.Tengeneza matuta yenye upana wa mita 1 na urefu wowote
kutegemea na mahitaji yako.Weka mbolea ya samadi ndoo moja hadi mbili
kwa mraba wa mita moja.
Lima tuta kiasi cha sentimita 10-25.
Sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya
sentimita 15 kutoka mstari hadi mstari Katika upandaji wa mstari mbegu
hupandwa katika nafasi ya sm 10 hadi 15 kati ya mstari na mstari. Gramu 5
(kijiko cha chai) zinatosha kusia eneo la mraba mita moja.
Tandaza nyasi na mwagilia.
Baada ya kupanda mbegu hufunikwa na
udongo mwepesi na baadaye matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu
kuota matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe
ili kuiwekea kivuli miche michanga. Mbegu za vitunguu huota baada ya
siku 7 hadi 10.
KUMBUKA KAMA UNATAKA KUWA MKULIMA NA ULIME ZAO LA VITUNGUU: Kilo 1.5 za mbegu zinatosha hekari moja ya shamba.
KUPANDIKIZA MICHE BUSTANINI(kutoka kwenye kitalu kwenda shambani)
Upandikizaji wa miche ya vitunguu
hufanyika baada ya miche kukua na kufikia unene wa Penseli. Mara nyingi
miche hii hukaa kwenye kitalu kwa siku 40 baada ya kupandwa.
Usichelewe kuhamishia miche yako
bustanini maana ukipandikiza miche mikubwa itaanza kutoa maua badala ya
kitunguu (bulbs). Hivyo mara nyingi miche ya namna hii hubaki na suke la
maua.
Wakati wa kupandikiza usikate wala
kupunguza majani. Miche ipandikizwe sm 30 kati ya mstari na mstari na sm
10 kati ya mche na mche.
Upandaji katika bustani hufanyika kwenye
mistari katika matuta au kwenye vijaruba. Vijaruba hutumika katika
maeneo tambarare na yenye ukame ili kuhifadhi unyevu baada ya
kumwagilia. Sehemu zenye udongo mzito na wenye maji mengi tumia matuta
yenye mwinuko wa sm 10 hadi sm 15 kutoka usawa wa ardhi.
KUMBUKA: Pandikiza miche wakati wa asubuhi au jioni na mwagilia maji ya kutosha lakini hakikisha maji hayatuami.
UWEKAJI WA MBOLEA
Weka mbolea ya kukuzia katika wiki ya
nne hadi sita baada ya kupandikiza. Weka mbolea kwenye mstari na
hakikisha isigusane na mimea. Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha
wakati wa kuweka mbolea. Tumia UREA au SA.
Zao la vitunguu linahitaji maji katika kipindi chote cha ukuaji wa mmea na hasa wakati wa utungaji wa tunguu (bulb).
Katika kipindi kisicho na mvua, miezi ya
mei hadi Agost, umwagiliaji ufanyike mara moja kwa wiki Pia katika
umwagiaji hutegemea sana na aina ya udongo katika shamba lako kwa sisi
wataalamu kama tunajua aina ya udongo uliopo shambani kwako tutaweza
kukuambia inatakiwa umwagilie kwa muda gani na unatakiwa umwagilie tena
baada ya siku ngapi.
Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu,
unashauriwa kupunguza kiasi cha maji kadri vitunguu vinapoendelea kukua.
Pia ni vema uache kumwagilia maji wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna.
Kwani muda kamili wa kukomaa vitunguu na kuvuna ni siku 90 hadi 120
kutegemeana na aina ya mbegu.
KUDHIBITI MAGUGU(PALIZI) NA KUPANDISHIA UDONGO.
Kitunguu ni zao lisiloweza kuvumilia
magugu, magugu husababisha kupungua kwa ukubwa wa kitunguu, hueneza
magonjwa na husababisha kudumaa kwa kitunguu.
Katika bustani ya vitunguu, magugu
yanaweza kung'olewa kwa kutumia jembe dogo la mkono, kung'olea kwa mkono
au kwa kutumia madawa ya kuulia magugu (herbicides).
KUMBUKA: Unapotifulia, epuka kutifua kwa
kina kirefu maana utaharibu udongo na vitunguu vyenyewe kwa kuwa mizizi
ya vitunguu ipo juu juu sana.
Kupandishia udongo kwenye mashina ya
vitunguu ni hatua muhimu ili vitunguu visiunguzwe na jua. Hakikisha
kwamba mashina ya vitunguu vyako yako ndani walau sm 5. Pia kuna aina
nyingine ya vitunguu ambavyo hutoa au hupandisha tunguu lake juu ya
udongo vinapokua. Hivyo kupandishia udongo ili kufunika tunguu ni muhimu
sana.
Hakikisha shamba linakuwa safi. Wakati
wa kupalili, mkulima asichimbue sana udongo ili kuepuka mikwaruzano
kwenye shina la vitunguu. Inulia udongo kwenye mashina kama mkulima
amepanda sesa.
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU.
Wadudu waharibifu.
Kuna aina mbili za wadudu wanaoharibu hili zao;
1. Viroboto wa vitunguu
Hawa ni wadudu waharibifu namba moja wa
zao vitunguu hapa nchini kwetu Tanzania. Husababisha upotevu mkubwa
wakati wa mavuno. Wadudu hawa huonekana hasa kipindi cha joto.
Dalili.
Majani yaliyoshambuliwa na wadudu hawa
huwa na mabaka meupe yenye kung'aa. Katika hali iliyokithiri majani yote
huwa na tabaka jeupe au kijivu na baadaye hunyauka kabisa.
Kuzuia.
Mdudu huyu huzuiwa kwa kupiga dawa ya kuulia wadudu (insecticide) kama vile Marathion, Thiodan-35, Parathion
Ili kupunguza uvamizi mkubwa panga kupanda vitunguu mapema ili kipindi cha joto kinapofika kikute vitunguu vyako vimekomaa.
Epuka kupanda vitunguu katika shamba lililokuwa limepandwa jamii ya vitunguu hapo kabla kama vile liksi, vitunguu swaumu, n.k.
3. Bungua weupe (White grub)
Huyu ni aina ya funza mkubwa,. Hutaga
mayai yake kwenye uozo wa majani na samadi na hivyo mashamba
ya vitunguu yaliyoko karibu hata kwenye maeneo au mashamba karibu huwa kwenye hatari
zaidi. Mdudu huyu huathiri
kitunguu kwa kukata miche na minyoo wa vitunguu.
Hushambulia mizizi na kusababisha kukauka kwa
mimea.
Kutifulia shamba na kuwaweka wazi
wadudu hawa kunapunguza idadi yao.
Pia Hawa huzuiwa kwa kuzingatia mzunguko wa mazao
MAGONJWA.
Ugonjwa huu huonekana wakati wa baridi ulioambatana na unyevu mwingi angani.
Dalili.
* Utaona unga unga wa rangi ya zambarau katika majani.
* Majani hugeuka rangi na kuwa ya njano na kisha hunyauka.
* Ugonjwa huu hupenya hadi chini kwenye tunguu na husababisha kuoza.
KUZUIA
Fanya kilimo cha mzunguko ukihakikisha
unapanda mazao mengine yasiyo jamii ya vitunguu. Panda vitunguu tena
baada ya miaka mitatu kama athari ilikuwa kubwa.
Tumia dawa za ukungu (fungicides)
kunyunyizia katika shamba. Hii ifanyike kabla ya dalili kuonekana. Tumia
dawa kama Zineb ya unga, Maneb, Dithane M45, n.k.
Wakati unapoona dalili za hali ya hewa
yenye baridi ikiambatana unyevunyevu angani. Katika kipindi hiki piga
dawa kila baada ya siku sita ili kuzuia ugonjwa kuingia.
Ugonjwa ukishaingia kwenye mmea hauzuiliki kwani hakuna dawa ya kuponesha.
2. Ukungu wa kahawia.
Ugonjwa huu huleta madhara makubwa wakati vitunguu vikiwa bustanini na hata wakati vitunguu viko ghalani.
Dalili.
Vikovu
mbonyeo hujitokeza kwenye majani na baadaye huwa na rangi ya zambarau.
Vikovu hivi hukua na kutengeneza vidonda ambavyo hukua na kufanya
mzunguko katika jani zima au katika shina la kitunguu. Baada ya wiki
kama tatu tangu kuingia kwa ugonjwa huu, majani yote huanguka na kidmsha
kukauka.
Ugonjwa huu hushambulia kitunguu hata
baada ya kuvuna kupitia sehemu ya shingo ya kitunguu au sehemu yoyote
yenye kovu, kidonda au mkwaruzo.
NAMNA YA KUZUIA
*Katika bustani, unapoona kitunguu kina dalili ya ugonjwa huu, ng'oa na choma.
* Kwa kinga ya bustani, piga dawa za
Dithane M45 na dawa zingine za ukungu. Dawa hizi hupunguza uwezekano wa
kuenea kwa ugonjwa huu.
* Tumia kilimo cha mzunguko wa mazao katika eneo la bustani yako. Usipande vitunguu katika mzunguko wa jamii ya vitunguu.
* Wakati wa kuvuna epuka kukata vitunguu na kusababisha vidonda na makovu.
* Ukishavuna anika kwa siku mbili kabla ya kuhifadhi kwenye magunia.
3. Ugonjwa wa kuoza mizizi
Huu ni ugonjwa unaotoka udongoni na huenezwa na vimelea vya Ukungu (fungi).
Dalili
Mizizi kugeuka rangi na kuwa njano na kisha zambarau. Baada ya muda ugonjwa huenea na mizizi hufa kwa kunyauka.
KUZUIA
Panda vitunguu kwa mzunguko wa mazao. Epuka kurudia kupanda vitunguu kwa mfululizo.
Panda aina za mbegu zinazostahilimili magonjwa kama;
Excel, L36, Granex, White Granex, Red creole.
4. Ugonjwa wa doa la pinki (Purple blotch)
Uanza kama doa dogo linalozama ndani ya jani na kisha
linaongezeka ukubwa na kufanya rangi ya pinki. Kiini cha ugonjwa
huu huanzia kwenye mbegu na pia hubaki kwenye maozo ya majani
ya vitunguu. Aina ya Red Creole inaonyesha kutoshambuliwa sana
na ugonjwa huu.
Ugonjwa wa doa la pinki Kuoza kwa kitunguu
Mbinu za kudhibiti ugonjwa huu ni kuendesha mzunguko (crop
rotation) wa muda mrefu wa mazao pamoja na kuzuia kutuama kwa
maji shambani. Kupunguza msongamano wa mazao shambani na
matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium
hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine,
matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu
uongeza mlipuko wa magonjwa. Viatilifu kama vile Mancozeb
hutumika kuzuia mashmbulizi ya ugonjwa huu.
Vitunguu hustawi maeneo yasiyo na mvua
nyingi sana, yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na maeneo yasiyo na
joto kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaa kwa vitunguu.
Vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo
wenye rutuba ya kutosha, unaoruhusu mizizi kupenya na unaohifadhi unyevu
kama vile udongo wa nusu mfinyanzi nusu tifutifu.
UPANDAJI WA MBEGU ZA VITUNGUU KWENYE KITALU.
Hapa kwetu Tanzania upandaji huanza
mwezi March hadi Mei kutegemea na msimu wa kilimo ulivyo. Hivyo kilimo
hiki huanza mara baada ya mvua kubwa za masika kumalizika. Kipindi cha
kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri wa vitunguu.
Mbegu za vitunguu huoteshwa mapema
katika kitalu. Mbegu zinaweza kutawanywa au kupandwa kwa mistari katika
tuta la kitalu.Tengeneza matuta yenye upana wa mita 1 na urefu wowote
kutegemea na mahitaji yako.Weka mbolea ya samadi ndoo moja hadi mbili
kwa mraba wa mita moja.
Lima tuta kiasi cha sentimita 10-25.
Sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya
sentimita 15 kutoka mstari hadi mstari Katika upandaji wa mstari mbegu
hupandwa katika nafasi ya sm 10 hadi 15 kati ya mstari na mstari. Gramu 5
(kijiko cha chai) zinatosha kusia eneo la mraba mita moja.
Tandaza nyasi na mwagilia.
Baada ya kupanda mbegu hufunikwa na
udongo mwepesi na baadaye matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu
kuota matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe
ili kuiwekea kivuli miche michanga. Mbegu za vitunguu huota baada ya
siku 7 hadi 10.
KUPANDIKIZA MICHE BUSTANINI(kutoka kwenye kitalu kwenda shambani)
Upandikizaji wa miche ya vitunguu
hufanyika baada ya miche kukua na kufikia unene wa Penseli. Mara nyingi
miche hii hukaa kwenye kitalu kwa siku 40 baada ya kupandwa.
Usichelewe kuhamishia miche yako
bustanini maana ukipandikiza miche mikubwa itaanza kutoa maua badala ya
kitunguu (bulbs). Hivyo mara nyingi miche ya namna hii hubaki na suke la
maua.
Wakati wa kupandikiza usikate wala
kupunguza majani. Miche ipandikizwe sm 30 kati ya mstari na mstari na sm
10 kati ya mche na mche.
Upandaji katika bustani hufanyika kwenye
mistari katika matuta au kwenye vijaruba. Vijaruba hutumika katika
maeneo tambarare na yenye ukame ili kuhifadhi unyevu baada ya
kumwagilia. Sehemu zenye udongo mzito na wenye maji mengi tumia matuta
yenye mwinuko wa sm 10 hadi sm 15 kutoka usawa wa ardhi.
Zao la vitunguu linahitaji maji katika kipindi chote cha ukuaji wa mmea na hasa wakati wa utungaji wa tunguu (bulb).
Katika kipindi kisicho na mvua, miezi ya
mei hadi Agost, umwagiliaji ufanyike mara moja kwa wiki Pia katika
umwagiaji hutegemea sana na aina ya udongo katika shamba lako kwa sisi
wataalamu kama tunajua aina ya udongo uliopo shambani kwako tutaweza
kukuambia inatakiwa umwagilie kwa muda gani na unatakiwa umwagilie tena
baada ya siku ngapi.
Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu,
unashauriwa kupunguza kiasi cha maji kadri vitunguu vinapoendelea kukua.
Pia ni vema uache kumwagilia maji wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna.
Kwani muda kamili wa kukomaa vitunguu na kuvuna ni siku 90 hadi 120
kutegemeana na aina ya mbegu.
KUDHIBITI MAGUGU(PALIZI) NA KUPANDISHIA UDONGO.
Kitunguu ni zao lisiloweza kuvumilia
magugu, magugu husababisha kupungua kwa ukubwa wa kitunguu, hueneza
magonjwa na husababisha kudumaa kwa kitunguu.
Katika bustani ya vitunguu, magugu
yanaweza kung'olewa kwa kutumia jembe dogo la mkono, kung'olea kwa mkono
au kwa kutumia madawa ya kuulia magugu (herbicides).
KUMBUKA: Unapotifulia, epuka kutifua kwa
kina kirefu maana utaharibu udongo na vitunguu vyenyewe kwa kuwa mizizi
ya vitunguu ipo juu juu sana.
Kupandishia udongo kwenye mashina ya
vitunguu ni hatua muhimu ili vitunguu visiunguzwe na jua. Hakikisha
kwamba mashina ya vitunguu vyako yako ndani walau sm 5. Pia kuna aina
nyingine ya vitunguu ambavyo hutoa au hupandisha tunguu lake juu ya
udongo vinapokua. Hivyo kupandishia udongo ili kufunika tunguu ni muhimu
sana.
Hakikisha shamba linakuwa safi. Wakati
wa kupalili, mkulima asichimbue sana udongo ili kuepuka mikwaruzano
kwenye shina la vitunguu. Inulia udongo kwenye mashina kama mkulima
amepanda sesa.
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU.
Wadudu waharibifu.
Kuna aina mbili za wadudu wanaoharibu hili zao;
1. Viroboto wa vitunguu
Hawa ni wadudu waharibifu namba moja wa
zao vitunguu hapa nchini kwetu Tanzania. Husababisha upotevu mkubwa
wakati wa mavuno. Wadudu hawa huonekana hasa kipindi cha joto.
Dalili.
Majani yaliyoshambuliwa na wadudu hawa
huwa na mabaka meupe yenye kung'aa. Katika hali iliyokithiri majani yote
huwa na tabaka jeupe au kijivu na baadaye hunyauka kabisa.
Kuzuia.
Mdudu huyu huzuiwa kwa kupiga dawa ya kuulia wadudu (insecticide) kama vile Marathion, Thiodan-35, Parathion
Ili kupunguza uvamizi mkubwa panga kupanda vitunguu mapema ili kipindi cha joto kinapofika kikute vitunguu vyako vimekomaa.
Epuka kupanda vitunguu katika shamba lililokuwa limepandwa jamii ya vitunguu hapo kabla kama vile liksi, vitunguu swaumu, n.k.
3. Bungua weupe (White grub)
Huyu ni aina ya funza mkubwa,. Hutaga
mayai yake kwenye uozo wa majani na samadi na hivyo mashamba
ya vitunguu yaliyoko karibu hata kwenye maeneo au mashamba karibu huwa kwenye hatari
zaidi. Mdudu huyu huathiri
kitunguu kwa kukata miche na minyoo wa vitunguu.
Hushambulia mizizi na kusababisha kukauka kwa mimea.
Hushambulia mizizi na kusababisha kukauka kwa mimea.
Kutifulia shamba na kuwaweka wazi
wadudu hawa kunapunguza idadi yao.
Pia Hawa huzuiwa kwa kuzingatia mzunguko wa mazao
MAGONJWA.
Ugonjwa huu huonekana wakati wa baridi ulioambatana na unyevu mwingi angani.
Dalili.
* Utaona unga unga wa rangi ya zambarau katika majani.
* Majani hugeuka rangi na kuwa ya njano na kisha hunyauka.
* Ugonjwa huu hupenya hadi chini kwenye tunguu na husababisha kuoza.
KUZUIA
Fanya kilimo cha mzunguko ukihakikisha
unapanda mazao mengine yasiyo jamii ya vitunguu. Panda vitunguu tena
baada ya miaka mitatu kama athari ilikuwa kubwa.
Tumia dawa za ukungu (fungicides)
kunyunyizia katika shamba. Hii ifanyike kabla ya dalili kuonekana. Tumia
dawa kama Zineb ya unga, Maneb, Dithane M45, n.k.
Wakati unapoona dalili za hali ya hewa
yenye baridi ikiambatana unyevunyevu angani. Katika kipindi hiki piga
dawa kila baada ya siku sita ili kuzuia ugonjwa kuingia.
Ugonjwa ukishaingia kwenye mmea hauzuiliki kwani hakuna dawa ya kuponesha.
2. Ukungu wa kahawia.
Ugonjwa huu huleta madhara makubwa wakati vitunguu vikiwa bustanini na hata wakati vitunguu viko ghalani.
Dalili.
Vikovu
mbonyeo hujitokeza kwenye majani na baadaye huwa na rangi ya zambarau.
Vikovu hivi hukua na kutengeneza vidonda ambavyo hukua na kufanya
mzunguko katika jani zima au katika shina la kitunguu. Baada ya wiki
kama tatu tangu kuingia kwa ugonjwa huu, majani yote huanguka na kidmsha
kukauka.
Ugonjwa huu hushambulia kitunguu hata
baada ya kuvuna kupitia sehemu ya shingo ya kitunguu au sehemu yoyote
yenye kovu, kidonda au mkwaruzo.
NAMNA YA KUZUIA
*Katika bustani, unapoona kitunguu kina dalili ya ugonjwa huu, ng'oa na choma.
* Kwa kinga ya bustani, piga dawa za
Dithane M45 na dawa zingine za ukungu. Dawa hizi hupunguza uwezekano wa
kuenea kwa ugonjwa huu.
* Tumia kilimo cha mzunguko wa mazao katika eneo la bustani yako. Usipande vitunguu katika mzunguko wa jamii ya vitunguu.
* Wakati wa kuvuna epuka kukata vitunguu na kusababisha vidonda na makovu.
* Ukishavuna anika kwa siku mbili kabla ya kuhifadhi kwenye magunia.
3. Ugonjwa wa kuoza mizizi
Huu ni ugonjwa unaotoka udongoni na huenezwa na vimelea vya Ukungu (fungi).
Dalili
Mizizi kugeuka rangi na kuwa njano na kisha zambarau. Baada ya muda ugonjwa huenea na mizizi hufa kwa kunyauka.
KUZUIA
Panda vitunguu kwa mzunguko wa mazao. Epuka kurudia kupanda vitunguu kwa mfululizo.
Panda aina za mbegu zinazostahilimili magonjwa kama;
Excel, L36, Granex, White Granex, Red creole.
Uanza kama doa dogo linalozama ndani ya jani na kisha
linaongezeka ukubwa na kufanya rangi ya pinki. Kiini cha ugonjwa
huu huanzia kwenye mbegu na pia hubaki kwenye maozo ya majani
ya vitunguu. Aina ya Red Creole inaonyesha kutoshambuliwa sana
na ugonjwa huu.
Ugonjwa wa doa la pinki Kuoza kwa kitunguu
Mbinu za kudhibiti ugonjwa huu ni kuendesha mzunguko (crop
rotation) wa muda mrefu wa mazao pamoja na kuzuia kutuama kwa
maji shambani. Kupunguza msongamano wa mazao shambani na
matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium
hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine,
matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu
uongeza mlipuko wa magonjwa. Viatilifu kama vile Mancozeb
hutumika kuzuia mashmbulizi ya ugonjwa huu.linaongezeka ukubwa na kufanya rangi ya pinki. Kiini cha ugonjwa
huu huanzia kwenye mbegu na pia hubaki kwenye maozo ya majani
ya vitunguu. Aina ya Red Creole inaonyesha kutoshambuliwa sana
na ugonjwa huu.
Ugonjwa wa doa la pinki Kuoza kwa kitunguu
Mbinu za kudhibiti ugonjwa huu ni kuendesha mzunguko (crop
rotation) wa muda mrefu wa mazao pamoja na kuzuia kutuama kwa
maji shambani. Kupunguza msongamano wa mazao shambani na
matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium
hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine,
matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu
uongeza mlipuko wa magonjwa. Viatilifu kama vile Mancozeb
UVUNAJI WA VITUNGUU
Kwa ujumla uvunaji wa vitunguu huanza
siku 90 hadi 150 tangu kwa miche kupandwa yaani miezi mitatu hadi mitano
tangu kupandikizwa bustanini kutegemeana na mbegu iliyopandwa.
Utagundua kuwa vitunguu vyako viko tayari kuvunwa unapoona karibu 50% au zaidi ya mazao shambani yanaanguka au majani kukauka.
Ili kurahisisha ukaushaji wa vitunguu, pangilia muda wako ili uvunaji ukutane na kipindi cha joto na kiangazi.
Uvunaji ufanywe kwa kung'oa baada ya kumwagilia maji bustani siku moja kabla ya kuvuna.
Baada ya kuvuna, kata majani sm 2 juu na
kata mizizi sm 2 chini. Usikate chini sana ya shingo maana husababisha
jeraha na kupelekea kitunguu kuoza.
KUMBUKA:Ucheleweshaji wa uvunaji
unasababisha vitunguu kuoza na kuharibikia shambani. pia Tumia jembe la
mkono na hakikisha vitunguu havikwaruzwi wakati wa kuvuna. Unaweza
kuvuna tani 30-40 kwa hekta.
Octavian Justine Lasway
Irrigation and Water resources Engineer

Reviewed by BENSON
on
October 04, 2017
Rating:
No comments