KILIMO BORA CHA MINAZI.
UPANDAJI
Uko wa ina mbili kuna wa vibox na wa pembetatu lakini kwa aina zote mbili
umbali wa kupanda ni mita 7.6 kutoka shimo hadi shimo la mnazi, kiasi cha
mashimo 175 kwa hecta huingia na kama utatumia mtindo wa pembetatu basi mashimo
13 zaidi yataingia kwa hecta.
Ukubwa wa shimo uwe futi tatu kwa kina, upana na urefu hi kwa maeneo yenye
udongo mzuri na wakaida lakini maeneo yenye changarawe, mawe mawe na miamba
ukubwa uongezeke hadi futi4 kwa mapana , urefu na kina, Shimo lijazwe majani
kiasi cha kilo 15 – 20 unaweza kukisia kama theluthi moja ya shimo au futi moja
baada ya kushindilia majani, weka juu yake kama, weka udongo wa juu (top soil)
kiasi cha futi moja tena ongezea kiasi cha kilo 10 – 20 cha mbolea ya samadi.
Hakikisha haijai na kufunika shimo lote, pia kama utapata ule udongo mwekundu
ambao wengi hupenda kuutumia kwenye bustani zao, pia weka humu kiasi kama
utaukosa basi acha vivo hivyo, anza kumwagilia maji wiki moja kabla ya kupanda
mbegu yako, kama shimo litatitia ongezea udongo wenye rutuba ya kutosha,
kumbuka kuacha kisahani kwa ajili ya kukusanyia maji, ila kama ni sehemu ambazo
hufurika kipindi cha mvua jaza udongo hadi kuweka tuta ili maji
yasituame.
UPANDAJI
Ni vizuri kutumia mbegu ya nazi moja kwa moja kuliko kutumia miche, hii ni kwa
sababu mbili kubwa, kwanza ukinunua mche unakuwa hujui imetoka mnazi gani,
wenye ubora gani na hata uzaaji wake huujui, lakini inashauriwa kununua nazi
kutoka kwenye mnazi moja kwa moja kwa kuchagua mnazi bora na unaozaa nazi
nyingi na kubwa, chagua nazi kubwa zaidi kutoka katika kila mnzi bora.
Nazi ambayo haijafuliwa inakuwa na pembe tatu, moja ya pembe hizi huwa kubwa
zaidi na mbili zilizobaki hufanan ukubwa, ule upande mkubwa ulazwe chini wakati
wa kupandwa, na upande ule wenye kikonyo ambako nazi hujishika katika matawi ya
mnazi (mahanda) ndipo ambapo huota, utatakiwa upatate au upapunguze kwa kisu
ili kurahisisha kuota, wakati wa kupanda hakikisha nazi ina maji, ikiwa na maji
kidogo sana usiipande, panda miezi miwili au mitatu kabla ya mvua kuanza, nazi
inauwezo wa kuota yenyewe bila mvua kwa sababu ina maji ndani yake, ila baada ya
kuanza kuota kama hakuna mvua ni muhimu kumwagilia ama sivyo mbegu yako
itakufa.
Pia ni muhimu kutumia dawa za kuua mchwa au oil chafu wakati wa kupanda, pia
kunadaadhi ya mimea ambayo mizizi yake hufukuza mchwa inaweza kupandwa pamoja
na nazi yako. Kama utaamua kutumia miche basi hakikisha miche yako haipungui
umri wa miezi sita tangu mbegu kupandwa ili kuzuia miche mingi kufa.
MAGONJWA YA MINAZI
KUOZA VIKONYO
Huanza kwa majani machanga mawili ya mwanzo kubadilika rangi na kuwa njano na
baadae huwa na vidoti vyeusi hutokea kwenye ukingo, majani hunyauka na kukauka
na kisha sehemu ya chini linapoanzia jani huoza na kutoa harufu mbaya ambapo
baadae mnazi wote hufa.
Ili kuzuia ugonjwa huu mara tu unapoona dalili za mwanzo tengeneza mchanganyiko
ufuatao (gramu 100 za copper sulphate changanya na nusu lita ya maji) + (Gramu
100 za chokaa changanya na nusu lita ya maji) kila moja itengenezwe peke yake
halafu kisha vichanganywe pamoja baadae kisha pulizia kwenye minazi iliyoanza
kushambuliwa, kama mnazi umeshambuliwa sana ukatwe na kuchomwa moto kuzuia
maambukizi zaidi. Pia pulizia mchanganyiko huu msimu wa baridi kuanzi mwezi wa
5 hadi wa 9 kwenye shamba lako kama kinga.
KUOZA MAJANI
Majani huwa meusi kwenye ukingo na kuti likiliwa zaidi kati kati, majani
machanga yakichomoza huwa dhaifu na kisha huchanguka, mnazi haufi ila mazao
huwa duni kama ni mnazi unaozaa
ili kuzuia tumia dawa yoyote ya kuzuia fangasi za mimea kama Hexaconazol,
Mancozeb au Dithane - M5, muhimu ukufika duka la pembejeo ulizia dawa ya kuua
fangasi wa mimea utapata dawa na maelekezo ya kuchanganya usikariri haya majina
ya dawa nilizotaja
KILIMO BORA CHA MINAZI.
Reviewed by BENSON
on
September 29, 2017
Rating:
No comments