KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO
Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi
zinazoendelea. viazi husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300
hadi 2700 juu ya usawa wa bahari. hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi
mitano.
viazi mviringo vina virutubisho vingi mfano vitamin, protin,madini
SIFA ZA MBEGU BORA ZA VIAZI
·
Zenye
kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja
·
ziwe
zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi zaidi ya manne
·
zisiwe
na wadudu pamoja na magonjwa
·
zitoke
katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ukungu na mnyauko
·
zenye
ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la kuku
AINA
BORA YA VIAZI MVIRINGO
Kuna
aina nyingi sana ya viazi mviringo lakini hapa nitataja aina ambazo nazifahamu
na ni bora
kutoka
taasisi ya utafiti wa kilimo uyole
·
baraka
·
sasamua
·
tana
·
subira(EAI
2329)
·
Bulongwa
·
kikondo(CIP
720050)
MUDA
WA KUPANDA
Viazi mviringo mara nyingi katika maeneo mengi vinapandwa agost hadi september
na november hadi December. Natumia sentimita 60 hadi 75 kutoka mstari hadi
mstari na nafasi kati ya kiazi na kiazi ni sentimita 30.
MBOLEA
Ili kupata mazao mengi kutoka shambani mkulima anashauriwa kutumia mbolea aina
ya samadi, mboji, maan mabichi na za viwandani
kwa mbolea za viwandani tumia kilo 300 au mifuko 6 za mbolea ya TSP kwa hekta
moja, ns kilo 300 mifuko 6 za mbolea ya CAN au kilo 400 mifuko 8 ya SA au kilo
175 mifuko 3.5 za UREA.
PALIZI
Palilia viazi wiki mbili au tatu baada ya kuchomoza. inulia udongo kufanya tuta
zuri ili pawepo na unyevu wa kutosha na kufunika viazi kutokana na mwanga wa
jua
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
Ili kuzuia ugonjwa wa ukungu tumia Ridomil. changanya gram 100 za dawa
katika lita 20 za maji na nyunyuzia mara baada kila wiki mbili au tatu
kutegemea na hali ya hewa.
nyunyuzia dawa ya karate kiasi cha mililita 20 mpaka 40 za dawa katika lita 20
za maji ili kuzuia wadudu kama inzi weupe na wengine. Tumia mbinu bora za
kilimo kama usafi wa shamba au kilimo mzunguko kama mbinu ya kuzuia magonjwa na
wadudu.
KUVUNA NA MAVUNO
Viazi huwa tayari kuvunwa baada ya miezi 3 hadi 5 kutoka kupanda. mda
wa kuvuna unategemea na mda wa kupanda na dhumuni la zao
usiache viazi shamban bila kufunika kwa nyasi au udongo kwa mda
mrefu
KUHIFADHI
Viazi vya chakula viiafadhiwe kwenye ghara hewa ya kutosha pasiwe na
unyevunyevu na joto kali
KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO
Reviewed by BENSON
on
September 28, 2017
Rating:
No comments