JINSI YA KUSINDIKA MBOGA ZA MAJANI KWA NJIA YA UKAUSHAJI
Ukashauji wa mboga
za majani ni njia ambayo inatumika sana maeneo ya vijijini lakini si vibaya
ikianza pia kutumika maeneo ya mijini kwani ni njia nzuri sana. Kwa maneno
mengine njia hii ni usindikaji wa mboga za majani. Na moja kati faida kubwa
ambayo utaipata mara baada ya kukausha mboga hizi ni kwamba mboga hizi zinaweza
kukaa kwa muda mrefu hivyo kusaidia wakati wa mboga zinapokuwa hadimu.
Mambo ya msingi ya
kuzingatia wakati wa kukusha mboga za majani ni ifuatavyo:
1.
Chuma mboga nyingi katika bustani
yako. Hajalishi ni mboga za aina gani.
2.
Hatua inayofuata ikatekate vipande
vidogo vidogo.
3. Baada ya hapo chemsha katika maji
ya moto. Lakini jambo la kuzingatia ni kwamba chemsha mpaka ibadili rangi yake,
isiwe katika hali ya ukijani.
4.
Mara baada ya kuchemka na
kujiridhisha kwamba imeiva vizuri. Epuka kisha subiri kwa muda fulani mpaka
ipoe vizuri.
5.
Ikisha poa vizuri chukua kitu ambacho kitakusaidia kuianika
mboga hiyo mpaka ikauke vizuri.
6.
Mara baada ya kukauka vizuri ni
kwamba unaweza ukaiifadhi sehemu safi ili ije kuliwa hapo baadae.
JINSI YA KUSINDIKA MBOGA ZA MAJANI KWA NJIA YA UKAUSHAJI
Reviewed by BENSON
on
August 14, 2017
Rating:
No comments