ZIFAHAMU AINA KUMI (10) ZA SUNGURA
1. New Zealand Whites: Hii ni jamii mojawapo
maarufu kwa ufugaji wa sungura wa nyama, na kwa nchi kama Marekani, nyama yake
ndiyo bora zaidi kuliko aina nyingine za sungura. Sungura hawa wanaweza
kufikisha kilogramu 3.6 hadi 5.
2. Californian
Rabbits: Hawa ni uzao chotara wa sungura jamii ya Chinchilla na New Zealand
Whites. Wana manyoya meupe na madoa meusi na wanafahamika kutokana na maumbile
yao kama matofali na wanatoa nyama nzuri. Wanaweza kufikisha kilogramu kati ya
3.2 hadi 4.8.
3. American Chinchilla : Hawa ni aina bora
ya sungura kwa ajili ya nyama na wanarandana na sungura jamii ya Chinchilla
ambao hata hivyo ni wakubwa kwa maumbo. Wana rangi ya kijivu na nyama yao
inaweza kufikisha hadi kilogramu 3.6. Nyama yake inapendelewa Zaidi kukaangwa
ama kubanikwa.
4. Silver Foxes: Hawa ni sungura rafiki
zaidi kufugwa majumbani ambao wanafaa kwa mapambo pamoja na nyama. Aina hii ni
adimu sana na wanaweza kufikisha kilogramu kati ya 4 hadi 5. Wana rangi ya
fedha yenye kivuli cheusi na masikio yeliyoinuka, kama alivyo mbweha wa rangi ya
fedha.
5. Champagne D Argent:
Aina hii ya sungura wa kihistoria anayevutia imetumiwa kwa nyama tangu mwaka
1631. Nyama yao inapendwa ulimwenguni kote na ni wazuri kwa kufugwa. Unaweza
kuwakuta katika rangi mbalimbali kama nyeupe, rangi ya maziwa au chocolate.
6. Cinnamons:
Hawa ni uzao chotara kati ya sungura wa New Zealand White na American
Chinchilla. Maumbile yao yamerandana na asili yao. Sungura hawa wanatoa nyama
nzuri na wanafugwa zaidi kibiashara kwa ajili ya nyama.
7. Satins: Hawa ni
sungura wakubwa na wazito ambao wanatoa kiwango kikubwa cha nyama. Ni wazuri
kwa kufugwa kwa ajili ya nyama. Maumbile yao ni ya kati na wanapatikana katika
rangi mbalimbali kama bluu, nyeusi, shaba, chocolate, nyekundu, Siame na otta.
8. Rex: Sungura
hawa wenye manyoya laini yanayoteleza hufugwa kwa ajili ya manyoya na nyama.
Wanapokuwa wakubwa wanaweza kufikisha kati ya kilogramu 3.2 hadi 4. Wana rangi
za bluu, amber na madoa meupe. Nyama yao ni nzuri na wanafaa sana kufugwa.
9. Palomino: Hawa ni jamii bora ya
nyama na wanafugwa kibiashara kwa ajili ya nyama tu. Ni wapole na wanafaa
kufugwa nyumbani. Wanaweza kufikisha kati ya kilogramu 3.2 hadi 4.5.
10. Flemish Giants:
hawa ni sungura wakubwa na mabanda yao lazima yajengwe kwa ukubwa wa mita moja
urefu.Ukubwa kamili hufikiwa bada ya miezi 9. Hawazaliani kwa haraka lakini
wanaweza fikisha watoto 12 kwa mzao mmoja. Sungura
aina ya 01,02,03 na 09 tayari wanapatikana Tanzania katika mikoa ya Arusha, DSM
na Kilimanjaro.
ZIFAHAMU AINA KUMI (10) ZA SUNGURA
Reviewed by BENSON
on
June 13, 2018
Rating:
No comments