YAFAHAMU MAGONJWA YA KUKU KIUNDANI ZAIDI NA JINSI YA KUYATIBU.

Image result for magonjwa ya kuku
Siku ya leo tutaendelea na kwa kuangalia magonjwa mengine  ya kuku ambayo hutibika kwa dawa kama ifuatayo:

 1.KUHARA DAMU (coccidiosis)
 Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

Dalili. 

  • Kuku huzubaa na kujikunyata
  • Kuku kuharisha kinyesi chenye damu au kinyesi cha kahawia
  • Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na kulegea mabawa na kuonekana kama wawevaa koti
  • Kuku hupungukiwa homa ya kula
  • Vifo huwa vingi kwa vifaranga

Tiba ya ugonjwa huu.Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium, au Basulfa.

Kinga za ugonjwa huu.Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu unyevuunyevu katika banda la kuku.

2. HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)
        Husababishwa na bakteria

 Dalili za ugonjwa huu ni;

  •    Kuku hupata homa kali
  •    Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano
  •    Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye wiki 1-2
  •    Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya miguu,kuchechemea,kukosa hamu ya kula
  •    Kuku wanaotaga hupunguza utagaji,hutaga mayai yenye ganda laini na hupata   vifo vya ghafla

 Tiba za ugonjwa huu.
  Dawa za oxytetracycline kama Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu.

 Kinga za ugonjwa huu.
  Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji kwa kuku.
  Tenganisha kuku wagonjwa na wazima

3. MINYOO
Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga

 Dalili za ugonjwa huu
  • Kuku hukonda
  • Kuku huarisha
  • Kuku hukohoa
  • Kuku hupunguza utagaji
  • Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri
  • Kuku hupungua uzito

Tiba za ugonjwa huu.
Tumia dawa za minyoo kama piperazine

Kinga za ugonjwa huu.
Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila baada ya miezi mitatu

4.VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI
   Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo kwa wingi kwa vifaranga Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani kwa sana lakini nao huathiriwa sana.

Dalili za ugonjwa huu.

  •  Kuku kutochangamka
  •  Ukuaji mdogo wa kuku
  •  Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa na chawa,utitiri au  viroboto
  •  Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu

Tiba za ugonjwa huu
Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na mabanda yao.

Kinga za ugonjwa huu.


 Boresha usafi wa mabanda ya kuku.
YAFAHAMU MAGONJWA YA KUKU KIUNDANI ZAIDI NA JINSI YA KUYATIBU. YAFAHAMU MAGONJWA YA KUKU KIUNDANI ZAIDI  NA JINSI YA KUYATIBU. Reviewed by BENSON on June 14, 2018 Rating: 5

No comments