MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATUA WAKATI WA UANDAAJI WA KITALU CHA NYANYA


Related image
Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.

Yafuatayo ndiyo mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa uandaaji wa vitalu vya nyanya.

• Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche].

• Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.

• Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.

• Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo.

• Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba.

• Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota.
MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATUA WAKATI WA UANDAAJI WA KITALU CHA NYANYA MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATUA WAKATI WA UANDAAJI WA KITALU CHA NYANYA Reviewed by BENSON on June 04, 2018 Rating: 5

No comments