MATUTA YA MCHICHA YANATAKIWA KUWA HIVI
Tuta la Mchicha linatakuwa liwe na umbo kama hilo pichani (umbo la kaburi). Hata mvua ikinyesha au maji yakizidi tuta halituamishi maji, mchicha hauozi maana maji yaliyozidi hutiririka kutoka nje ya Tuta.
Pia Tuta la dizaini hii husaidia mizizi ya mchicha kupenya vizuri ardhini hivyo kupata mchicha wenye afya zaidi.
Kumbuka! Kama unafanya kilimo cha mchicha kibiashara hakikisha unapanda mchicha kwa kupishanisha (rotation).Mfano kama una matuta 15,Usipande matuta yote siku moja, unaweza ukapanda matuta 3 na kila baada ya siku 3 unapanda mengine matatu ili uweze kusambaza ya mboga zako bila kuishiwa .
MATUTA YA MCHICHA YANATAKIWA KUWA HIVI
Reviewed by BENSON
on
May 01, 2018
Rating:
No comments