FAIDA ZA MBOLEA YA MBOJI
Matumizi ya mbolea ya mboji katika kilimo cha mazao yana faida zifuatazo;
- Utengenezaji wa mbolea ya mboji hauna gharama na ni rahisi hivyo wakulima wa ngazi zote wanaweza kuumudu.
- Mbolea ya mboji huboresha muundo wa udongo unaopelekea kuwa na mzunguko mzuri wa hewa na maji katika udongo.
- Mbolea ya mboji huongeza virutubisho vinavyohitajika na mmea katika udongo na hivyo kuongeza mazao.
- Mboji huongeza uwezo wa udongo kutunza maji na hivyo kupunguza kasi ya ukaukaji wa udongo hasa katika maeneo yenye hali ya joto na yasiyopata mvua za kutosha.
- Mbolea ya mboji huweza kutumika kama mbadala wa mbolea ya samadi wakati wakuandaa kitalu cha mboga.
- Mbolea ya mboji huboresha afya ya mmea na kufanya uwe na uwezo wa kustahimili magonjwa.
FAIDA ZA MBOLEA YA MBOJI
Reviewed by BENSON
on
April 30, 2018
Rating:
No comments