JINSI YA KUDHIBITI VIWAVIJESHI KWA KUTUMIA VIUTILIFU.

Kiwavijeshi Vamizi ajulikanae kama Fall Armyworm au kwa jina la kitaalamu “Spodoptera frugipedra” asili yake ni Bara la America. Mdudu alionekana kwa mara ya kwanza katika nchi za Africa Magharibi (Nigeria) mwishoni mwa mwaka 2016.

Hadi mwezi February 2017, kiwavijeshi huyu alikuwa ameshavamia nchi za Afrika Kusini, Kati na Mashariki zikiwemo Zimbabwe, Msumbiji, Zambia, Congo na Rwanda
Hapa nchini kiwavijeshi vamizi aliripotiwa kwa mara ya kwanza katika wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa mwezi Machi 2017.

Hadi mwezi Disemba 2017 kiwavijeshi huyu alisharipotiwa kwenye mikoa zaidi ya 15 Maarufu kwa kilimo cha mahindi ikiwemo Mbeya, Shinyanga,Ruvuma, Iringa, Geita, Manyara,Arusha, Kilimanjaro, Morogoro,Tanga, Kigoma, Kagera,Mwanza,Pwani na Lindi.
Udhibiti wa kutumia Viuatilifu

  • Kagua shamba kubaini uwepo wa lava wa Kiwavijeshi Vamizi kwenye shamba
  • Tumia viatilifu vilivyosajiliwa Tanzania kwa kufuata maelekezo kwenye kibandiko kilichopo kwenye kifungashio.
  • Kiuatilifu kipulizwe wakati wa asubuhi au jioni kwenye eneo lililoshambuliwa na Kiwavijeshi Vamizi
  • Kwa ushauri unaweza kutumia kiuatilifu chenye usajili wa jina la DUDUBA EC, Belt 480SC, Emamectin benzoate au Mupacron 50EC, DUDUALL, PROFECRON n.k
  • Matumizi ya kiuatilifu iwe ni hatua ya mwisho baada ya mbinu nyingine kushindwa
JINSI YA KUDHIBITI VIWAVIJESHI KWA KUTUMIA VIUTILIFU. JINSI YA KUDHIBITI VIWAVIJESHI KWA KUTUMIA VIUTILIFU. Reviewed by BENSON on May 24, 2018 Rating: 5

No comments