HIZI NDIZO AINA YA NYANYA UNAZOWEZA KUHIFADHI MUDA MREFU BILA KUHARIBIKA
a) Tengeru’97 ambayo ina sifa vifuatazo:
- Huzaa sana kutokana na wingi wa matunda na muda mrefu wa kuvuna, ambao hufikia michumo mikubwa kati ya 6-7 kuanzia kuvuna hadi mwisho wa mavuno.
- Aina hii ina sifa ya kuwa na ganda gumu, hivyo haziharibiki haraka wakati wa kusafirisha au kuhifadhi (wastani wa siku 20)
- Zina sifa ya kuvumilia baadhi ya magonjwa kama vile ugonjwa wa kunyauka
- Tengeru’97 hustahimili mashambulizi ya minyoo fundo (Root knot nematodes)
b) Tanya
- Sifa kubwa ya Tanya ni kwamba nayo huzaa sana
- Huwa na ganda/ngozi ngumu ambayo inazuia kuoza au kuharibika kwa urahisi wakati wa kusafirisha au wakati wa kuhifadhi kwa muda mrefu.
- Tanya nayo ina ladha nzuri inayopendelewa na walaji wengi
Zingatia: Tatizo la Tanya na T97 ni kwamba si kubwa sana kama marglobe 2009. Lakini ukubwa ni karibu unge karibiana, haujapishana sana. Kwa ujumla, ukubwa na wingi wa mazao hutegemea sana matunzo, udongo, hali ya hewa na mazingira kwa ujumla.
HIZI NDIZO AINA YA NYANYA UNAZOWEZA KUHIFADHI MUDA MREFU BILA KUHARIBIKA
Reviewed by BENSON
on
May 30, 2018
Rating:
No comments