JINSI YA KUSIA MBEGU ZA NYANYA KATIKA KITALU
Mbegu za nyanya huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye huhamishiwa shambani.Matayarisho ya kitalu hufanyika wiki 1 au 2 kabla ya kusia mbegu. Tengeneza tuta lenye upana wa mita 1 na urefu wa kuanzia mita 5 hadi urefu unaoweza kuhudumia kwa urahisi. Vunja mabonge makubwa kwa kutumia jembena kulainisha udongo vizuri.Changanya mbolea za asili zilizooza vizuri kama vile Samadi au mboji kiasi cha debe 1- 2 katika eneo la mita mraba 1.
Sawazisha kwa kutumia reki au kifaa kingine. Mwagilia kitalu siku moja kabla ya kusia, kisha sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya sentimita 10 – 15 kutoka mstari hadi mstari.
Kiasi kinachotosha eneo la mita mraba 1 ni gramu 3 – 5 (sawa na nusu kijiko cha chai hadi kimoja) Kiasi hiki cha mbegu huweza kutoa miche inayoweza kutosha kupandikiza katika eneo la mita mraba 100. Kiasi cha mbegu kinachohitajika kwa hekta 1 ni gramu 300.
Weka matandazo kama vile nyasi kavu na kasha mwagilia maji asubuhi na jioni mpaka mbegu zitakapoota.Mbegu huota baada ya siku 5 – 10. Ondoa matandazo baada ya mbegu kuota na endelea kumwagilia maji hadi miche itakapofikia kupandikizwa.Jenga kichanja ili kzuia jua kali na matone ya mvua yasiweze kuharibu miche michanga.
JINSI YA KUSIA MBEGU ZA NYANYA KATIKA KITALU
Reviewed by BENSON
on
May 29, 2018
Rating:
No comments