KANUNI ZA MSSINGI KATIKA KILIMO CHA DENGU

Image result for kilimo cha dengu

Faida ya zao la Dengu

  • Chakula chenye viini lishe vya protini 
  • Mboga, bajia/vitafunwa


  • Huongeza kipato na _hupunguza umasikini 
  • Hurutubisha udongo 
  • Huifadhi unyevu aridhini
  • Chakula chenye viini lishe vya protini 
  • Hutumika kama Mboga, kutengenezea bajia/vitafunwa


Kwa kuwa na uwezo wa kuvumilia maji kidogo Dengu Huongeza kipato na na utajiri

  • Hhurutubisha udongo 
  • Huhifadhi unyevu ardhini


Utayarishaji wa shamba
Shamba litayarishwe kwenye mvua za mwishoni baada ya kuvuna mpunga/mahindi
1. Lima mara ya kwanza sm 15 (plough), rudia mara ya pili (harrow) ondoa miti, majani, mawe na mabonge ya udongo
2. Lima kwa trekta, jembe la kukokotwa na ng’ombe/wanyama au jembe la mkono

Maandalizi ya mbegu
Aina za mbegu na upatikanaji …..kuna Mbegu ya awali, msingi, kuazimiwa

  • Mbegu za dengu hazihitaji mvua nyingi kwenye kuotesha na kukuza
  • Unyevu uliopo shambani baada ya kuvuna mazao mengine unatosha
  • Husitawi vizuri kwenye mbuga ambapo maji hayatuami


Aina za dengu zilizothibitiswa na kufanyiwa utafiti Tanzania
Mwanza 1 

  1. ni aina ya Desi rangi yake ni kahawia maua yake pia ni kahawia
  2. Mavuno ni mpaka 950kg/hekta ama ekari 2.5 
  3. Kukomaa siku 83


Ukiriguru 1

  • Ni aina ya Desi rangi ya mbegu ni kahawia, maua zambarau
  • Kukomaa siku 93
  • mavuno koala 1000 kg/hekta/2.5 ekari


Mbegu za Dengu

  1. Mwanza 2 Aina ya Kabuli


  • Mbegu za rangi ya maziwa, maua meupe
  • Mavuno 1000 – 1500kg/hekta/2.5 ekari
  • Hukomaa siku 90


Mangaza Aina ya kabuli

  • Kukomaa siku87
  • _Mavuno mpaka kg 1000 kwa hekta/ekari 2.5


Upandaji wa mbegu shambani

  • Mbegu zenye matawi kidogo: 
  • Msitari hadi msitari ni sentimeta 30 na shimo hadi shimo sentimeta 10′


Mbegu zenye matawi mengi

  • Msitari hadi msitari ni sentimeta 40 na shimo hadi shimo sentimeta 20

Muda mrefu na kati: 

  • Panda mbegu 2 kwa kila shimo


Baada ya wiki 6 kulingana na majani shambani, palilia 
-Palizi hupunguza ushindani wa chakula, mwanga na mazalia ya wadudu

Kudhibiti visumbufu mimea shambani
Wadudu waharibifu:

  • Wana tabia ya kufyonza kwenye majani, matawi, mashina, maua hata mbegu hasa zikiwa changa kama vitunda. 
  • Wenye tabia ya kukata mashina na kuangusha mimea michanga na wengine hutafuna majani na maua. 
  • Funza wanaotoboa matunda/vitumba


Kudhibiti visumbufu mimea shambani

  • Chawa weusi au wa kijani (aphids) chini ya majani au kwenye shina:



  • Tumia viua tilifu au viua dudu pindi unapoona mashambulizi shambani°


Funza wanaotoboa vitumba:

°Nyunyizia viua tilifu au viua dudu pindi vitumba vya maua vinapoanza kufunga, rudia mara ya pili baada ya siku 10 -14 mara ya 3 itategemea wadudu shambani°

Kudhibiti visumbufu Dengu shambani
Dawa zinazopendekezwa
#LAMDA CYHALOTHRIN MF karate: changanya cc 40 kwenye lita 15 za maji
changanya cc 40 kwenye lita 1 ya ULVA
#Amerate: changanya cc 40 kwenye lita 15 za maji
#Profecron: changanya cc 40 kwenye lita 15 za maji.

Kudhibiti Mafinga sumbufu dengu shambani
Mnyauko Fuzari Fusarium wilt (fusarium spp)
Husababishwa na aina ya vimelea (fungus). Vimelea huishi kwenye udongo na mbegu pia kwenye mabaki au tabaka za mimea zilizooza kwenye udongo.

Dalili: 

  • Kulegea kwa majani na kuelekea chini
  • Mmea kunyauka na kufa kabisa Weusi katikati ya shina likipasuliwa


Kuzuia: 

  • Kilimo mzunguko wa mazao
  • Panda mbegu zinazostahimili ugonjwa
  • zingatia usafi wa shamba


Uvunaji

  • Unashauriwa kuvuna una mapema mimea inapokuwa imekomaa vizuri
  • Epuka kuchelewa/ukichelewa utapata hasara ya wadudu, panya, ndege na kupasuka kwa vitumba

Maelekezo ya kuvuna

  • Vuna mojamoja au ng’oa shina zima na sambaza kwenye eneo lililoandaliwa
  • Kisha anika mbegu kwenye jua siku 2 kabla ya kupiga


  • Hifadhi kwenye eneo lenye hewa nyingi


KANUNI ZA MSSINGI KATIKA KILIMO CHA DENGU KANUNI ZA MSSINGI KATIKA KILIMO CHA DENGU Reviewed by BENSON on April 05, 2018 Rating: 5

No comments