KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI
KANUNI YA KWANZA – KUTAYARISHA SHAMBA MAPEMA
- Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita.
- Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.
- Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.
FAIDA YA KUANDAA SHAMBA MAPEMA
- Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.
- Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
- Hupunguza magugu.
- Hupunguza wadudu waharibifu.
KANUNI YA PILI ; kujua wakati wa kupanda mbegu sahambani.
Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki, Kama mvua hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako.
- Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni.
- Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati
- Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni
- Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni.
Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua.
Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu, panya, ndege na wanyama wengineo.
FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA
- Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
- Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.
- c) Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.
KANUNI YA TATU KUCHAGUA MBEGU BORA
Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
- a) Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
- b) Huzaa mazao mengi.
- c) Hustahimili magonjwa.
AINA ZA MBEGU
- Mbegu aina ya chotara (hybrid)
- Aina ya ndugu moja (synthetic)
- Mbegu aina ya composite
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta moja au umi kwa hekari.
MAPENDEKEZO YA MBEGU ZA KUPANDA
Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa
SIDCO ,PANNAR, CHOTARA, kutoka KENYA n.k Ni vyema
kufuata ushauriwa wataalamu wa kilimo
Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikazidi
- Mazao hupungua.
- Mmea huangushwa na upepo
- Mabua mengi hayazai.
Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu.
KIASI CHA KUPANDA
- Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali(sumu
- Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja., (Hii hutegemea na aina ya mbegu)
Nafasi za kupanda.
75cm x 30cm
75cm x 60cm
90cm x 25cm
90cm x 50cm
KANUNI YA TANO; KUTUMIA MBOLEA
Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwambolea pamoja na matunzo mengine ya kilimo bora. Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.
- Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hua na virutubisho vya kutosh ambavyo havijulikani vipo kwa kipimo kiasi gani
- Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na vipimo hujulikana, hii inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa kipindi gani.
KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI
Reviewed by BENSON
on
March 29, 2018
Rating:
No comments