KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI
Moja kati mbinu ambazo zitakufanya uweze kulima kilimo
chenye tija kujua kanuni ambazo zitakuzaidia kuweza kulima kilimo hicho, na
kanunia hizo nitazieleze katika Makala haya. Mahindi ni zao muhimu linalo limwa
katika maeneo ya kitropiki. Pia zao hili hulimwa katika udongo wenye uchachu pH
6-6.5. lakini pia hustawi zaidi kwenye maeneo yenye mwinuko wa 2500.
KANUNI YA KWANZA; Kutayarisha
shamba mapema.
a) Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna
mazao ya msimu uliopita.
b) Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba
na usiosimamisha maji.
c) Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.
Faida ya kuandaa shamba mapema
1. Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika
kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.
2. Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
3. Hupunguza magugu.
4. Hupunguza wadudu
waharibifu.
KANUNI YA PILI ; kujua wakati wa
kupanda mbegu sahambani.
Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki, Kama mvua hunyesha
nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za
kupanda zao la mahindi katika eneo lako.
1. Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi
Novemba hadi Desemba mwishoni.
2. Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati
hadi Februari katikati
3. Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba
hadi Desemba mwishoni
4. Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba
hadi Januari mwanzoni.
Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna
mazao mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe
wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua.
Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu, panya,
ndege na wanyama wengineo.
FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA
a) Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
b) Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa
milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.
c) Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi
vizuri.
KANUNI YA TATU KUCHAGUA MBEGU
BORA
Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
a) Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
b) Huzaa mazao mengi.
c) Hustahimili magonjwa.
AINA ZA MBEGU
a) Mbegu aina ya chotara(hybrid)
b) Aina ya ndugu moja(synthetic)
c) Mbegu aina ya composite
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri katika
misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta
moja au umi kwa hekari.
MAPENDEKEZO YA MBEGU ZA KUPANDA
Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano
wa
SIDCO ,PANNAR, CHOTARA, kutoka KENYA n.k Ni vyema
kufuata ushauriwa wataalamu wa kilimo
KANUNI YA NNE KUPANDA
Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikazidi
a) Mazao hupungua.
b) Mmea huangushwa na upepo
c) Mabua mengi hayazai.
Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa
mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu
katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu.
KIASI CHA KUPANDA
a) Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali(sumu
b) Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja., (Hii
hutegemea na aina ya mbegu)
Nafasi za kupanda.
75cm x 30cm
75cm x 60cm
90cm x 25cm
90cm x 50cm
KANUNI YA TANO; KUTUMIA MBOLEA
Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwambolea
pamoja na matunzo mengine ya kilimo bora. Ukipanda mbegu bora bila kutumia
mbolea ni kazi bure.
KUNA AINA MBILI KUU ZA MBOLEA
1. Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani
mabichi,mbolea hizi hua na virutubisho vya kutosh ambavyo havijulikani vipo kwa
kipimo kiasi gani
2. Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na vipimo
hujulikana, hii inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa kipindi gani.
KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI
Reviewed by BENSON
on
August 12, 2017
Rating:
No comments