JIFUNZE MATUNZO MAZURI KWA MBWA WA KUFUNGWA

Image result for MBWA

Mnyama huyu huaminika ndiye mwaminifu zaidi kati ya wanyama wote wanaofugwa nyumbani

Kuna wale wanaomfuga pia kwa sababu humchukulia kama 'kipenzi' chao (pet).
Je, wajua mbwa ni kitega uchumi kwa baadhi ya wanaomfuga? Mnyama huyu ametajirisha baadhi ya wafugaji wanaomthamini.
Mbwa hawa hufugwa na kutunzwa kwa msingi wa malengo matatu, wale wa kunusa (sneaver dogs), wa kulinda/kuhifadhi usalama (guard dogs) na wa kuongoza (guide dogs) maafisa wa usalama.
Mbwa huzaa mara mbili kwa mwaka ambapo hubeba ujauzito kwa kipindi cha siku 63 (miezi 2).
Kwa kawaida mbwa mmoja huzaa kati ya vilebu 8 - 12.
Lishe
Anachohitaji mbwa ni lishe bora pekee huku magonjwa yanayomwathiri yakiwa finyu kinyume na wanyama wengine.
"Lishe ni kiungo muhimu kwa mbwa, hulishwa kwa chakula anachokula binadamu japo kuna vyakula vingine vinavyonunuliwa kwenye maduka,".
Vilebu hulishwa mara mbili kwa siku huku walionenepa na kukomaa wakilishwa mara moja kwa siku.  Hulishwa kwa nyama, mifupa iliyosagwa, chakula halisi cha mbwa kinachojulikana kama 'Top dog', punje za mchele, samaki aina ya 'omena' ama masalia ya chakula.
"Chakula chake huchanganywa na vitamini mbalimbali (multi-vitamin) ili kuboresha afya yake, manyoya, meno na mifupa iwe dhabiti na yenye nguvu. Vitamini hivo ni: CAL-VITAMAX yenye madini ya Calcium'.
Ikumbukwe usafi wa makazi ya mbwa ni jambo la muhimu kuzingatia kwa minajili ya kufurusha wadudu kama vile viroboto na kupambana na magonjwa yanayotokana na uchafu.
"Makazi ya mbwa yanafaa kusafishwa na kupuliziwa kwa dawa aina ya dudu dust kila siku ili kufurusha viroboto. Kisha mbwa waoshwe kwa dawa aina ya Dudu Krin mara moja kwa wiki," ashauri, tabibu wa mifugo.
Magonjwa
Magonjwa kwa mbwa ni jambo linalofaa kutiliwa maanani wakati wa malezi yake. 
Magonjwa kama vile:
  •  Canine Distemper,
  •  Canine Herpatitis,
  •  Lep Tospirosis,
  •  Parvo Virus (ugonjwa wa kuendesha damu), 
  • Rabbies (Kichaa) ndio huathiri mbwa.
"Ili kuepuka athari za magonjwa haya hupewa aina tatu ya chanjo kwa mwaka. Kikubwa azaliwapo na kufikisha
  •  Wiki 6 hudungwa chanjo ya Parvo Virus, akiwa na umri wa 
  • Miezi 3 hudungwa ya DHLP na anapohitimu 
  • Miezi 4 hudungwa sindano ya chanjo ya Kichaa (Rabbies),
Kumbuka;Mbali na chanjo hiyo, pia hupewa dawa za minyoo (deworming) kila baada ya miezi 2. Dawa za minyoo hupewa kulingana na umri wa mbwa.
 Mbwa aliyefikisha umri wa mwezi mmoja na nusu hupewa nusu tembe ya dawa aina ya Plozin, miezi 6 hupewa tembe moja na aliye zaidi ya miezi minane hupewa tembe mbili.
"Kuna haja ya mbwa kuhusishwa kwenye matembezi ili kunyoosha viungo vyao vya mwili pia waweze wapunge hewa mwanana.

Faida kubwa
Usalama (security firms) na wanaowahifadhi kwa minajili ya kuimarisha usalama katika makazi yao na wanyama wa kucheza nao (pets).
JIFUNZE MATUNZO MAZURI KWA MBWA WA KUFUNGWA JIFUNZE MATUNZO MAZURI KWA MBWA WA KUFUNGWA Reviewed by BENSON on March 13, 2018 Rating: 5

No comments