FAHAMU MAMBO MAWILI KABLA HUJAANZA KILIMO BIASHARA
Habari
za leo ndugu msomaji wangu na pole kwa shughuri mbalimbali za
ujenzi wa Taifa. Jumatatu iliyopita nilikuandikia nilikuandikia makala
inayokufahamisha Kilimo bora cha zao la muhogo lakini leo nimekuletea
kitu cha tofauti kidogo. Unapoanzisha mradi unatarajia mwisho wa siku
uumalize kwa kupata faida, sasa basi leo nataka nikufahamishe mambo
makubwa mawili unayotakiwa kuyajua kabla hujaanza mradi wako wowote wa
kilimo.
Jambo la kwanza: Farming master-plan
Hili
ni jambo la kwanza na muhimu sana kulifahamu. Farming master-plan ni
muongozo wa shughuri zote unazotakiwa kuzifanya katika kilimo chako
tangu kuandaa shamba mpaka kuvuna. Hii ijumuishe shughuri kama kupanda,
kudhibiti magugu, uwekaji wa mbolea na kupulizia madawa ya wadudu na
magonjwa. Unatakiwa kujua shughuri hizi zote, muda wa kuzifanya, namna
ya kuzifanya na mahitaji yake ili uzifanye.
Kwa
mfano uwekaji wa mbolea: wakati gani uweke? kiasi gani? uwekeje?
Unatakiwa ufahamu haya yote kabla hujaanza mradi wako wa kilimo ilii
usipate usumbufu wakati wa utekelezaji.
Jambo la pili: Gharama za uzalishaji na makadirio ya faida
Hili
ni jambo lingine muhimu sana. Najua hujaamua kulima ili ujifurahishe
tu, unatafuta faida hivyo basi unatakiwa ujue mradi wako utakugharimu
kiasi gani katka utekelezaji wake na mwisho wa siku utakulipa kiasi
gani? Pengine hutopata gharama halisi lakini ni lazima ufahamuu japo
makadirio ya gharama ili kwanza uweze kujipanga lakini pia usikwame
katika utekelezaji wa mradi wako.
Kwanini ni muhimu kufahamu mambo haya?
- Utajua mahitaji muhimu unayotakiwa kuwa nayo kabla hujauanza mradi wa kilimo
- Utapata fursa ya kuuona mradi wako katika hatua mbalimbali hata kabla hujauanzisha
- Utaweza kujua makadirio ya gharama za uzalishaji na faida tarajiwa
Kwa hiyo nikunasihi ndugu yangu usianzishe mradi wako wa kilimo mpaka ujiridhishe kuwa unayafahmu mambo haya mawili.
FAHAMU MAMBO MAWILI KABLA HUJAANZA KILIMO BIASHARA
Reviewed by BENSON
on
March 05, 2018
Rating:
No comments