UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KUKU KWA KUTUMIA MCHWA.

Rafiki, mchwa na funza ni chakula bora sana kwa kuku. Chakula hiki kina protini kwa wingi sana kwa mifugo yetu, ili kuku aweze kukua vizuri na kuwa na uzito mzuri anahitaji vyakula vyenye protein kwa wingi.



Wadudu jamii ya funza na mchwa ni jamii ya wadudu ambao wana protin nyingi, iwapo kuku wako utawapa chakula hiki basi kuku wako watakuwa kwa haraka na watakuwa na uzito mkubwa ambao itakua ni faida kwako.



Pia chakula hiki cha mchwa na funza kinapunguza changamoto ya magonjwa kwa kiasi fulani hasa yale magonjwa yanayotokana na lishe. Mpaka hapo unaona faidaya wazi itokanayo na chakula hiki cha mchwa na funza.



1. UTENGENEZAJI WA FUNZA.
Ili uweze kutengeneza funza unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo; Nailon, samadi, maji na jembe na eneo la kutengenezea.
Jinsi ya kutengeneza funza;
Tengeneza tuta. 
1. Weka nailoni katika tuta lako.
2. Weka samadi yako (samadi mbichi ya Ng'ombe)
3. Weka udongo kwa mbali kwa juu katika samadi yako.
4. Mwagia mwagia maji, ninaposema mwagia mwagia maji namaanisha nyunyuzia maji katika tuta lako kwa kiasi kidogo.
5. Funika juu kwa nailoni katika eneo ambalo umetengeneza tuta lako hakikisha kusiwe na jua kali.
6. Katika tuta lako hakikisha kunakuwa na unyevu unyevu.
7. Baada ya siku kumi funua nailoni lako utakuta kunafunza wengi waache kuku wako wale hadi watakapomaliza.
8. Baada ya kumaliza kula funika tena na nailoni baada ya siku mbili utakuta tena kuna funza wakutosha hivyo unatakiwa utengeneze matuta mawili au zaidi kwa ajili ya chakula kwa mifugo yako,



2. UTENGENEZAJI WA MCHWA.
Ili kutengeneza mchwa unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo;
1. Samadi ya ng'ombe, maranda ya mbao au majani makavu au mabua mahindi,
Mabox au chungu.



Jinsi ya kutengeneza mchwa.
1. Chukua samadi ya ng'ombe changanya na maranda ya mbao vizuri mwagia maji michanganyiko wako ulowane vizuri.
2. Weka kwenye chungu au box michanganyiko wako.
3. Chukua chungu/box lako weka katika njia ya mchwa kwa maana sehemu yenye asili ya mchuguu ambapo mchwa wanapatikana.
4. Baada ya siku tatu utaona box lako linamejaa mchwa chukua ka wape kuku wako wale.
Hapa ndipo mwisho wa somo letu la leo natumaini umejifunza mengi katika somo la leo nenda kayafanyie kazi haya uliyojifujifunza ili kuboresha mifugo yako.




MUHIMU;- Chakula hiki kitumike kama chakula cha ziada.
Nikutakie utekelezaji mwema na tutaonana wakati ujao, usipange kukosa mfululizo wa makala hizi.
UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KUKU KWA KUTUMIA MCHWA. UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KUKU KWA KUTUMIA MCHWA. Reviewed by BENSON on January 27, 2018 Rating: 5

No comments