MFUGAJI WA SAMAKI, YAJUE MAGONJWA YA SAMAKI NA JINSI YA KUYATIBU.
Kuna magonjwa mengi ya samaki yanayosababishwa na fangasi,
bacteri protozoa, parasites, virus na mazingira yenyewe. Hapa nitajaribu
kuongelea magonjwa machache ambayo mimi ninauzoefu nayo yaani yameshanitoke na
nikapambana nayo
1. Ichthyosporidium (WHITE SPOTS)
Huu ugonjwa kwa kifupi hujulikana ka ICHI, husababishwa na fungus ambao huingia kwa kupitia ngozi na kisha kushambulia maini na figo.
Dalili zake ni samaki kuogelea kwa kupindapinda au kivivu, tumbo kuonekana kama halina kitu (hollow) n alama nyeupe nyeupe kwenye mwili w samaki.
Tiba yake ni pottasium per manganate kwenye maji, Phenoxethol 1% kwenye chakula na Chloromycetin kwenye chakula, da zote zinapatikana kwenye maduka (pet shops). kwa kawaida ICHI wana miznguko miwili ya maisha, akizaliwa anaogelea na kujishikiza kwenye mwili wa samaki, kisha anashuka chini kwen kuzaana (replitications)na kurudi kwen mwili wa samaki tena. Kwenye hatua hii pottasium per manganate ndio inafanya kazi ya kuzuia ICHI kurudi ten kwenye mwili wa samaki.
2. LEECHES
Ugonjwa huu husababishwa wadudu nje (external parasites ) ambao hujishiki kwenye mapezi na mikia ya samaki. Da yao ni kuwaona wakiwa wamejishikiza kwenye sehemu zilizotajwa na ndani y ngozi, huwa na umbo la kama moyo n rangi ya kijivu/nyeupe
Kwa sababu dalili zinaonekana wazi k macho, mara nyingi ugonjwa huu huin kwenye tank lako kwa njia ya konokon na majani.
Matibabu ni kuwaweka samaki ndani y maji yenye chumvi kiasi cha asilimia 2. baada ya dakika 15 leeches wengi watakuwa wamedondoka chini na wale watakaobaki unaweza kuwatoa kwa kutumia kibanio (forceps).
Tiba nyingine ni kwa kutumia Trichlorofon kiasi cha 0.25m/l (robo miligram kwa lita moja ya maji) majani yanaweza kuondolewa ugonjwa kwa kutumia potassium permanganat e kiasi cha 5mg/l (miligram 5 kwa lita m ya maji)
3. KUOZA MKIA NA MAPEZI
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria , dalili zake kubwa ni kuwa rangi nyekundu au rangi ya udongo (hudhurungi) kama damu imevilia kwe kona za mapezi na mkia na kisha baad sehemu hizi hunyofoka na kubakia kibubutu.
Sababu kubwa ni kuumia kunakosababishwa na kujigonga au madume kupigana, TB pia inaweza kusababisha hali hii
Tiba yake ni kwa kutumia antibiotics kama tetracycline au chloramphenicol cha 20-30mg/l (miligramu 20-30 za da kwa lita moja ya maji)au mili gramu 25 (1 capsule) kwa chakula cha gramu 25, ingawa magonjwa mengi yanasababishwa na vimelea lakini mazingira nayo pia yanachangi katika kuongeza kasi ya magonjwa, ukizingati yafuatayo unaweza kuwakinga samaki wako.
(a) Nunua samaki wako toka kwa mtu mwenye uzoefu wa kufuga na ambaye unauhakika samaki wake hawana magonjwa.
(b) Samaki wapya watengwe kwa muda kwenye chombo kingine (hospital tank kwa siku kadhaa kabla ya kuchangany na wengine.
(c)hakikisha samaki wako hawali zaidi kiwango chao na kuvimbiwa, lisha kwa kipimo sahihi.
(d) Epuka kuwaweka samaki kwenye mazingira mabaya kama maji machafu, kuweka samaki wasiopatana pamoja, kuwasumbua kwa kuwashikashika na kugonga gonga tanki.
(e) Samaki wagonjwa watengwe kweny tank lingine (hospital tank).
(F) Nyavu zilizotumika kutolea samaki wagonjwa ziwekwe dawa (disinfection) zikaushwe juani na zioshwe vizuri hii n pamoja na tank na vitu vyake.
(g) hakikisha tank halina kitu chochote cha chuma (metal) na maji ya hospital tank yasiingie kwenye tank kuu
MFUGAJI WA SAMAKI, YAJUE MAGONJWA YA SAMAKI NA JINSI YA KUYATIBU.
Reviewed by BENSON
on
January 02, 2018
Rating:
No comments