YAJUE MATUNZO MUHIMU KWA KUKU WANAOKUA
Katika
matunzo ya kuku wanaokua, hapa tunaangalia mitemba au kuku wenye umri
wa kuanzia miezi miwili hadi minne. Kuku hawa wenye umri huu wanatakiwa
watunzwe vizuri ili wakusaidie kukupa mfugaji faida, vinginevyo
ukishindwa hapa kutunza kuku wako vizuri basi usitegemee kupata faida
kubwa.
1. Hatua ya 1, waweke kwenye banda kubwa.
Hatua
hii inakuja kama walikua bado kwenye eneo la kulea vifaranga, wahamishe
na uwapeleke kwenye banda kubwa. Kama banda ni hilo hilo moja,
waondolee ‘hardboards’ ulizokuwa umetengea vifaranga, na waachie kwenye
banda zima.
2. Hatua ya 2, wawekee bembea kwenye banda.
Ukumbuke
kwamba kuku ni ndege, hivyo kuna wakati wanapenda kuwa juu. Hivyo ni
muhimu kuwawekea bembea ili iwasaidie kufurahia maisha yao na kuwa huru
zaidi. Hiyo itakuwa ni sehemu mojawapo ya kufanya zoezi.
3. Hatua ya 3, weka matandazo safi.
Hakikisha
matandazo yasiwe na harufu kali au vumbi. Hakikisha pia maji
hayamwagiki bandani. Na Mara tu yakimwagika ondoa matandazo yaliyolowa
na weka mapya. Pia ukumbuke kubadilisha matandazo mapema ili yasiweze
kutoa halafu na kuleta magonjwa mengine yatakanayo na matandazo
kurundikana.
4. Hatua ya 4, weka ratiba ya usafi.
Unaweza
ukaweka ratiba ya usafi bandani na kwenye eneo la kuzunguka banda,
angalau mara mbili kwa wiki. Tumia dawa ya V-RID kufanyia usafi na
kupulizia dawa hewani. Hii itasaidia banda lako kubaki safi wakti wote
na afya kwa kuku wako pia.
5. Hatua ya 5, wape kuku maji safi muda wote.
Pia
unaweza kuwaongezea vitamin kwenye maji yao hasa kama wanafugwa ndani
muda wote. unapowapa maji safi muda wote si rahisi sana kuweza kupata
magonjwa yatokanayo na bakteria.
6. Hatua ya 6, wape chakula chenye virutubisho.
Usiwape
kuku wako ilimradi tu chakula, wape kuku wako chakula chenye
virutubisho vya kutosha. Unaweza ukaanza kuwapa ‘growers’ au aina
nyingine ya chakula kizuri. Ukiwalisha kuku wako chakula duni,
wanadumaa.
7. Hatua ya 7, rudia chanjo ya newcastle kwa wakati.
Hii
unaweza kufanya yaani kila baada ya wiki 10 tangu walipochanjwa mara ya
mwisho. Unaporudia chanjo inasaidia sana kuwafanya kuku wako wawe imara
wakati wote na inakuwa ngumu kukutana na magonjwa.
8. Hatua ya 8, wape dawa ya minyoo.
Dawa
ya minyoo unawapa kuku wakiwa na miezi miwili na rudia kila baada ya
wiki 10. Ukishindwa kuwapa dawa hii basi tegemea kuokota kuku wengi
ambao watakufa kutokana na kushambuliwa na minyoo.
9. Hatua ya 9, walishe majani na mboga mboga kwa wingi.
Unapowalisha
kuku majani ya mboga mboga hiyo itawairishia miili yao kwa kuiongezea
kinga dhidi ya magonjwa. Hata hivyo kama kuku wakilishwa majani ni
rahisi pia kuweza kutaga vizuri inapofikia kipindi hicho.
10. Hatua ya 10, kama una eneo kubwa, wafungulie nje ili wazunguke zunguke.
Waache
kuku wako wazunguke na waoge kwenye mchanga. Kuzunguka zunguka na
kuparua parua kunawafanya bize na kudonoana na kulana manyoya. Kuoga
kwenye mchanga kunawafanya wawe safi na kama wana wadudu, wanaweza
kuwaondoka.
11. Hatua ya 11, kuwa na mawasiliano ya karibu na daktari wa mifugo.
Mara tu uonapo dalili za ugonjwa, wasiliana na daktari wa mifugo kwa ushauri zaidi. Pia tafuta chanzo cha ugonjwa ili ukiondoe.
Mwisho wa somo letu la leo na tunaamini umejifunza kitu cha kukusaidia kuboresha ufugaji wako.
YAJUE MATUNZO MUHIMU KWA KUKU WANAOKUA
Reviewed by BENSON
on
December 21, 2017
Rating:
No comments