KWANINI NI MUHIMU KUTUMIA MBOLEA KATIKA KILIMO CHA MAHARAGE?
Wakulima wengi
wamekuwa wakipuuza huku baadhi yao wakiwa hwatambua kama ipo haja ya kutumia
mbolea katika kilimo hicho, ila ukweli ni kwamba maharage hayahitaji nitrogen
kwa wingi kwa sababu mizizi ya maharage husaidiana na viumbe hai (nitrogen
fixing bacteria) waishio kwenye udongo kutengeneza nitrogen.
Hata hivo maharage
yanahitaji phosphorus kwa ajili ya kuboresha mizizi na potassium kwa ajili ya
kuuandaa mmea kwa ajili ya kutoa maua mengi na kuzaa matunda bora.
Ikiwa shamba
lililimwa zao ambalo liliwekwa mbolea kama vile Urea au CAN basi huna haja ya
kuweka tena mbolea za nitrogen badala yake unaweza kuweka TSP au DAP Kg 60 kwa
hekta wakati wa kupanda. Au mbolea ya minjingu (Minjingu Rock Phosphate) Kg 250
kwa hekta moja wakati wa kupanda.
Kama shamba
limechoka sana au halikuwekwa mbolea za nitrogen msimu uliopita basi tumia NPK
katika uwiano wa 5:10:10 kiasi cha Kg 30 kwa hekta, nayo iwekwe wakati wa
kupanda. Mbolea zote ziwekwe sentimita tano hadi 10 kutoka kwenye shina/shimo
la mmea na urefu wa sentimita 3 hadi 5 kwenda chini.
Pia unaweza kutumia
mbolea ya zizi/samadi (tani 5 - 10 kwa hekta) au mbolea ya kijani (green
manure, tani 5 kwa hekta). Mwaga/tawanya samadi kwenye shamba lote halafu
ichangane vizuri na udongo kwa kulima kwa plau (la tractor au ng’ombe). Maana
yake ni kwamba mwaga samadi kabla ya kulima shamba lako kwa trekta/ng’ombe.
Mbolea ya kijani
inapatikana kwa kusafisha shamba halafu ukaliacha mpaka majani/magugu yakaota
kisha ukalilima kwa trekta au ng’ombe (likiwa na magugu hivyo hivyo) lakini
kabla hayajatoa mbegu halafu ukapanda. Mbolea ya minjingu inaweza kutumika
pamoja na samadi na mbolea ya kijani.
Lakini lincha ya
kueleza ya kwamba maharage yanahitaji mbolea kwa wingi kama ambavyo nimeeleza
hapo awali,
Maharage huhitaji mvua ya kutosha kipindi cha kabla ya uwekaji maua (before flowering) na kipindi cha ukuaji wa vitumba vya maharage (podding). Huhitaji unyevu kidogo kipindi cha kuweka maua (during flowering) na ukavu kipindi cha kukomaa (pod maturation) na kukauka vitumba. Vitumba ni matunda (pods). Ikiwa utatumia njia nyingine yoyote ya umwagiliaji angalia maharage yako yapo katika hatua gani kabla hujapanga ratiba yako ya umwagiliaji (irrigation schedule
KWANINI NI MUHIMU KUTUMIA MBOLEA KATIKA KILIMO CHA MAHARAGE?
Reviewed by BENSON
on
November 19, 2017
Rating:
No comments