KAMA UNAFUGA KUKU NA HUNA UHAKIKA KAMA WALISHAKWISHA KUPEWA CHANJO FANYA YAFUATAYO.
Inawezekana kuku ambao unawafuga umewanunua au
huna kumbukumbu kama walikwishapewa chanjo, kama ndivyo hivyo basi unachotakiwa
kufanya kwa sasa ni njia hii.
Kwanza uwape kuku wako antibiotic ili
kuwasaidia kuua magonjwa ya tumbo na mafua kama wanayo.
Hivyo
basi anza kuwapa dawa kwa mtiririko huu na nitakueleza kwanini.
1. Wape dawa hizi mbili kwa maramoja kisha
uchanganye na vitamin ya amin total.
A)Vitacox ya kepro uholanzi
B)Tylodox ya kepro uholanzi
C)Vitamin ya amin total
Dawa hizo hapo juu wape kwa maramoja yani
uzichanganye Kwenye maji zote tatu kwa maramoja.
Dozi
na vipimo
kama kuku wako wana uwezo wa kumaliza lita10
kwa siku basi weka vipimo hivi;
Weka maji Lita10, weka kijiko kimoja cha dawa
ya Vitacox, kijiko kimoja cha dawa ya Tylodox na kijiko kimoja cha vitamin ya
Amin Total. Changanya vizuri na uwape kuku wanywe siku nzima hayo maji yenye
mchanganyo wa hizo dawa. Na unatakiwa kuwapa dozi hiyo kwa mfululizo wa siku5
bila kuvusha hata siku moja.
kijiko kinachotumika kupima dawa hapo ni kile
kijiko cha chakula nasisitiza tumia kijiko cha chakula kila unachotumia kulia
wali.
Kama kuku wako hawamalizi maji ya lita10 kwa
siku basi weka maji lita5 na hapa unafata utaratibu huo huo kama hapo juu
nilivyoeleza. Isipokuwa tu kijiko utakachotumia kwenye maji ya lita5 ni kijiko
cha chai, kile kijiko kidogo kinachotumikaga kuwekea sukari kwenye chai kumbuka
ni kile kidogo sio cha chakula.
Lakini vipimo ni hivyo hivyo unaweka kijiko
kimoja kimoja cha kila dawa hapo tylodox kijiko kimoja, Vitacox kijiko kimoja
na vitamin ya amin total kijiko kimoja. Siku ni zile zile 5 mfululizo na maji
yaliyochamganywa yakae masaa24 (siku moja) kama hawajayamaliza mwaga na
uchanganye tena mengine yakiisha kabla ya muda changanya mengine kwa vipimo
hivyo hivyo
SABABU
ZA KUWAPA KUKU HIZO ANTIBIOTICS
1. Tunawapa Kuku hizo antibiotics ili kusaidia
kuondoa magonjwa ya tumbo na mfumo wa hewa (mafua na kifua) kama yapo kwa hao
kuku kabla ya kuwapa chanjo. Na hii ni kwasababu kuku ukimpa chanjo wakati ana
maambukizi ya magonjwa mengine mfano mafua,typhoid, kipindupindu, kuhara damu
na mengine ataumwa na kufa badala ya kupona, kumbuka chanjo hupewa kuku mzima
na sio magonjwa.
2. Baada ya kuku kumaliza dozi ya antibiotics
kaa siku tatu bila kuwapa dawa yoyote yani baada ya kumaliza siku 5 tangu
waanze hizo dawa za awali kaa siku tatu ya nne uwape dawa ya minyoo. Siku ya 9
uwape dawa ya minyoo.
3. Baada ya kuwapa dawa ya minyoo
wakamaliza kaa kwa muda wa siku 7 bila
kuwapa dawa yoyote(wiki moja) Siku inayofuata baada ya wiki kupita ndio sasa
uwape chanjo ya mdonde
5.Baada ya kuwapa chanjo ya mdonde unakaa tena
wiki moja bila kuwapa dawa yoyote siku inayofuata unawapa *lchanjo ya gumboro
Ukimaliza mzunguko huo kuku wako watakuwa wapo
salama kabisa ila utatakiwa kurudia chanjo kila baada ya miezi mitatu kupita
KAMA UNAFUGA KUKU NA HUNA UHAKIKA KAMA WALISHAKWISHA KUPEWA CHANJO FANYA YAFUATAYO.
Reviewed by BENSON
on
November 18, 2017
Rating:
No comments