ZIJUE KANUNI BORA ZA KILIMO CHA MIPAPAI
Miongoni kati kilimo ambacho kinalipa
kwa hivi sasa ni kilimo cha mapapi. kama
mtu ataamua kulima kilimo bora cha
mapapi kwa kuzingatia kanuni zifutazo basi mtu huyo ajiandae kupata faida
lukuki,
Mambo ya muhimu ya kuzingatia hasa
pale unapotaka kulima kilimo hiki ni;
MAHITAJI
Hali ya hewa inayofaa kwa mipapai ni ya kitropik ambayo
haina baridi kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha maji maji yakisimama kwa
masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya kutosha kwa
sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu, kipindi cha
jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji
kama hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii
huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni
Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani
huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga
upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena
Spp) na miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu
kuzidi mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi
Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza
kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe
zao hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa.
Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya
michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti
na mboga mboga yanaweza kulimwa. Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai
dume, majike na yenye jinsia zote(multiplesex/hermaphrodite) ambayo
huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai
mafupi sana
MBEGU
Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na
kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za kununua
ni vizuri zaidi, baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja
KUOTESHA MBEGU
Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia
miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu
zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo wenye rutuba au
pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 – 27 na itachukua
kati ya wiki 1 – 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 – 3. Panda
mbegu zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na
sentimeta 15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza
kupiga dawa ya copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji
ilikukinga miche yako na fangasi
UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA
Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya
kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga
mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 – 5 kila shimo maana miche
mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume
KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU
Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20
– 40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa
sentimeta 40 – 60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana
na sentimeta 30 kina na shimo lichanganywe na udongo na samadi
bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni mita 3 kwa 3 kwani
mipapai inahitaji jua la kutosha
KUPUNGUZA MIPAPAI
Baada ya miezi 3 – 5 baada ya kupanda mipapai
itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe
na hasa midume, mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 – 20 na midume
ibaki mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi
ing’olewe
RUTUBA YA UDONGO
Weka kiasi chakilo 2 – 5 za samadi kwenye kila
mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia
kuwekwa kama matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia
unyevu usipotee.
MAGUGU
Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili
kuzuia uoataji wa magugu, magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua
chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka matandazo
kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu
UANGALIZI
·
Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au
kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya
fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako.
·
Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na
hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
·
Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha
yale yenye afya tu.
·
Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa
wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike.
·
Mipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya
mazao bora ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani
mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe
ZIJUE KANUNI BORA ZA KILIMO CHA MIPAPAI
Reviewed by BENSON
on
October 23, 2017
Rating:
No comments