JAMBO LA MUHIMU SANA UNALOTAKIWA KULIJUA KABLA YA KUANZA KUFUGA KUKU.
Unapotaka kujikita katika suala la ufugaji wa
kuku ipo haja kubwa ya kuweza kufikiria ni kwanama gani utaweza kuwa mfugaji
bora wa kuku, Hii ni kwa wote, wafugaji na wanaotaka kuanza kufuga. Unapotaka
kuanza ufugaji unatakiwa uanze na ufugaji mdogo hata kama una mtaji mkubwa. Kwa
kufanya hivi itakusaidia kupata uzoefu katika nyanja zifuatazo:
1. Utunzaji.
Kwa kuanza na kiasi kidogo itakusaidia kujua ni ukubwa gani unafaa kwa kuku
wangapi, ukiwa na kuku wangapi utalisha chakula kiasi gani, pia utapata uzoefu
wa chanjo muhimu zinazohitajika hali ambayo itakurahisishia pindi utapoanza
ufugaji mkubwa.
2. Soko
Hapa tunalenga upatikanaji wa wateja wa bidhaa zako za mifugo, itakusaidia
kujua wateja waliopo wanavutiwa na bidhaa ya aina gani, kwa mfano mayai utajua
wanapenda mayai ya kiini cheupe au cha njano? Kwa kufaham wanchokihitaji utajua
ufanye nini ili ukidhi wanachokihitaji.
3.
Changamoto
Ukianza na ufugaji mdogo pia itakusaidia kujua changamoto zilizopo kwenye
ufugaji na utajifunza ni jinsi gani ya kuzitatua au kukabiliananazo kabla
ya kuanza ufugaji mkubwa.
Hivyo ni muhimu
kuweza kuyazingatia hayo ili uweze kuwa mfugaji mwenye mfagaji mwenye mafanikio
JAMBO LA MUHIMU SANA UNALOTAKIWA KULIJUA KABLA YA KUANZA KUFUGA KUKU.
Reviewed by BENSON
on
October 22, 2017
Rating:
No comments