HII NDIYO LISHE BORA KWA AJILI YA KUKU.
Mfugaji
ili uwape kuku wako lishe bora yenye kuendelea, na ili upate matokeo bora zaidi
katika ufugaji wako wa kuku basi yakupasa kuzingatia yafuatayo:-
- Tumia
chakula bora na siyo bora chakula. Tumia chakula bora ambacho hakina
madhara kwa kuku wako na hata walaji kwa ujumla.
- Weka
chakula mahali safi na salama kuepuka wadudu waharibifu kama vile panya
ili kuzuia maambukizi ya magonjwa kwa kuku.
- Tumia
kanuni ya "least cost combination" yaan tumia chakula cha
bei nafuu kinachotoa matokeo bora zaidi ili kupunguza gharama za ufugaji
hali ambayo itakufanya upate faida mara dufu.
Kwa kufanya hivyo utaweza kuwalisha
kuku wako chakula kilicho bora kwa matokeo bora zaidi bila kuyumba kiuchumi
wakati wote wa ufugaji wako.
HII NDIYO LISHE BORA KWA AJILI YA KUKU.
Reviewed by BENSON
on
October 21, 2017
Rating:
No comments