ZIJUE DALILI ZA UKOSEFU VITAMINI KATIKA KUKU.
Tofauti na aina nyingine ya vyakula
vya kuku, kama vile protini, wanga, mafuta, madini n.k ambavyo vinaweza
kutengenezwa mwilini, Ni vitamini K ambayo hutengenezwa katika utumbo wa kuku,
na vitamini C hutengenezwa na mwili wa kuku. Vitamini zingine hazitengenezwi
mwilini bali ni lazima kuku azipate kutoka kwenye chakula au apewe vitamini
zilizotengenezwa viwandani, na zinahitajika katika kiwango kidogo sana
mwilini.
Kuna makundi mawili ya vitamini, nayo ni:-
a/ Vitamini zinazoyeyuka kwenye
mafuta (fat soluble vitamins), ambazo ni vitamini A, D, E na K.
b/ Vitamini zinazoyeyuka kwenye maji
(water soluble vitamins) ambazo ni vitamini C, B1, B2, B12 na nyingine
nyingi.
Kuku huhitaji vitamini zote hizo
kwenye chakula, vitamini hizi zote ispokuwa moja (vitamini B12) zikizidi
mwilini huondolewa kupitia mkojo. Vitamini B12 inaweza kuhifadhiwa mwilini. Kwa
maana hiyo vitamini hizo ni lazima ziwe katika chakula kinacholiwa kila siku
(daily diet).
Maelezo haya yanaonesha kuwa kuku
anahitaji vitamini 14, kwani vitamini C hutengenezwa mwilini. Ingawa vitamini K
nayo hutengenezwa lakini haitoshelezi.
Vitamini C
Husaidia kifaranga kilicho ndani ya
yai kukua, mifupa ya kifaranga kuumbika na kukua vizuri, pia mafuta kusambaa
vizuri mwilini.
Viatamini A
Huhitajika kwa kiwango kidogo sana
katika chakula cha kuku, lakini kiasi hicho kidogo ni muhimu sana kwa kuku ili
aweze kukua, kutaga mayai mazuri, mayai yaanguliwe vizuri na macho yaweze kuona
vizuri.
Dalili za Upungufu wa vitamini A mwilini.
- Kuku
hukawia kukua.
- Kuku
huwa dhaifu na mwenye manyoya yasiyo na mpangilio.
- Macho
hayaoni vizuri.
- Utagaji
usioridhisha.
- Mayai
yatagwayo hayaanguliwi vizuri.
- Mayai
huwa na doa au madoa madoa ya damu ndani yake (blood spots in eggs)
- Kukishwa
kujikinga na maradhi ipasavyo.
- Kukonda.
- Manyoya
hayaoti ipasavyo (poor featherin
ZIJUE DALILI ZA UKOSEFU VITAMINI KATIKA KUKU.
Reviewed by BENSON
on
September 24, 2017
Rating:
No comments