JINSI VYURA, NDEGE NA WADUDU AMBAVYO HUBORESHA SHAMBA.
Mara nyingine sio kila mdudu au ndege
aliyo shambani kwako ni mwaribifu, wapo baadhi ya wadudu na ndege ni muhimu wawepo shambani ili waweze kulifanya
shamba liwe bora Zaidi. Hivyo katika Makala yetu ya leo nataka nikushinikishe
baadhi ya viumbe ambao ni muhimu wawepo shambani.
Mtu mwingine ataniuliza namalizaje kuwamalizaje
wadudu waharibifu shambani mwako bila kutumia dawa? Wala usipate tabu, ukweli ni kwamba wakati
mwingine usisahau kwamba zaidi ya kuwaua wadudu waharibifu, dawa hizo huua
viumbe muhimu kama vile minyoo na kuvu ambao ni muhimu sana katika
urutubishwaji wa udongo katika shamba.
Hivyo baadhi ya viumbe muhimu katika urutubishaji wa shamba ni
kama wafuatao:
1.
Vyura ni muhimu sana katika kilimo.
Chura anaweza kula wadudu waharibifu 10,000 kwa muda wa miezi mitatu naye
hachagui anachokula. Yeye hula viumbe wanaoharibu mimea kama vile nyenje,
wadudu na viwavi wa aina fulani, na konokono.
2.
Ndege pia hula viumbe waharibifu.
Kitabu Gardening Without Poisons chasema kwamba ndege aina ya wren alionekana
akiwalisha “makinda wake buibui na viwavi 500 alasiri moja katika majira ya
kiangazi.” Ukitaka ndege kadhaa aina ya wren au ndege wengine wanaokula wadudu
waje shambani mwako basi weka chakula cha ndege na vifaa vya kujenga kiota
mahala wanapoweza kuviona. Muda si muda, utaona wakija.
3.
Wadudu wengi wanaoboresha shamba hula
wadudu waharibifu. Ukinunua wadudu aina ya ladybug kisha uwaweke shambani
mwako, watawamaliza mara moja wadudu aina ya aphid kwani wanapenda kula wadudu
hao sana. Mayai ya kivunja-jungu yanaweza pia kununuliwa na kuwekwa shambani.
Mayai hayo yakianguliwa, vivunja-jungu
JINSI VYURA, NDEGE NA WADUDU AMBAVYO HUBORESHA SHAMBA.
Reviewed by BENSON
on
September 09, 2017
Rating:
No comments