NAMNA YA KUTAMBUA DUME MZURI KWA UZALISHAJI WA NG`OMBE WA MAZIWA.
Wafugaji wengi
wamekuwa wakipata ng’ombe wanaozalisha kidogo na kwa kiwango cha chini kutokana
na kuangalia ukubwa wa gharama ya mbegu wakidhania kuwa ndiyo upatikanaji wa
ng’ombe bora. Vinasaba husaidia kwa kiwango kikubwa katika kupata ng’ombe mzuri
wa maziwa.
Kuwepo kwa
ongezeko la uzalishaji wa maziwa hutegemeana na vitu viwili ambavyo ni
kuboresha mifugo kwa kufanya uchaguzi sahihi wa kizazi pamoja na usimamizi
mzuri unaojumuisha lishe kamili, malazi mazuri, upatikanaji wa maji,kuwa karibu
na wanyama pamoja na utoaji wa kinga na tiba dhidi ya magonjwa.
Vinasaba pamoja na
usimamizi mzuri ni vitu viwili vinavyotegemeana. Bila kuwa na uzao mzuri,
uzalishaji wa wanyama pamoja na usimamizi utakuwa wa hali ya chini sana, na
bila
usimamizi mzuri
wanyama bora hawawezi kuonesha ubora wao katika uzalishaji.
Uzao mzuri humpa
nafasi kubwa mfugaji kutambua sifa na uzalishaji utakaopatikana katika uzao
ujao. Endapo mfugaji atafanya uchaguzi mbaya basi ni hakika atakuwa na
uzalishaji hafifu wa maziwa, kuzorota kwa afya ya mnyama pamoja na maisha
mafupi.
Muda wa kufanya
tafiti
Wafugaji wengi
wamekuwa wakifikiria mbegu pale tu ng’ombe anapokuwa tayari anahitaji kupandwa
na matokeo yake ni kuwa, kutokana na haraka ya kutaka kumhudumia ng’ombe huyo,
basi mfugaji atakuwa tayari kuchukua mbegu yoyote ile atakoyopatiwa na
wataalamu. Kwa mantiki hiyo, hakuna muda mfugaji atatumia kuchunguza aina
ya dume aliyetumika kupatikana kwa mbegu hiyo na badala yake, gharama hutumika
kwa kiasi kikubwa kuonesha uwezo wa dume huyo.
Wafugaji wengi
hufikiri kuwa kitendo cha mbegu kuuzwa kwa gharama kubwa ni moja ya njia ya
kutambua ubora wa dume. Wauzaji wengi wamekuwa wakitumia njia hii kuwadanganya
na kuwarubuni wafugaji.
Ni muhimu sana kwa
mfugaji anaelenga kuzalisha maziwa kusoma na kuelewa taarifa zote muhimu
zilizotolewa kuhusu aina ya dume husika. Ili kufanikiwa katika uzalishaji wa
maziwa, ni muhimu kwa mfugaji kuwa makini na kulichukulia kwa uzito suala la
uchaguzi wa dume na kuelewa nini kinahitajika bila kubahatisha. Mfugaji ni
lazima atambue kuwa, dume huchangia asilimia 50 ya kinasaba katika uzao wake
hivyo ni muhimu sana kujua sifa za dume unayemchukua kwa ajili ya uzalishaji.
Pia ubora wa
maziwa huchangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya dume aliyetumika. Dume wa maziwa
hutambulika kwa kuangalia kiwango cha maziwa yanayozalishwa na ng’ombe
aliyepandwa na dume huyo na mtamba aliyezaliwa na ng’ombe huyo ambapo dume huyo
husambaza sifa ya maziwa kutoka kwa ng’ombe huyo hadi kwa mtamba.
Elewa maelekezo
yaliyopo kwenye kabrasha la mbegu
Kielelezo cha
vinasaba hutumika kupima uwezo wa mnyama kusambaza vinasaba vyake kwenda kwa
uzao ujao. Katalogi huwa na taarifa muhimu ambazo zitamsaidia mfugaji kufanya
uchaguzi mzuri wa dume ili kuwa na uhakika wa kuendeleza kizazi baada ya kingine.
NAMNA YA KUTAMBUA DUME MZURI KWA UZALISHAJI WA NG`OMBE WA MAZIWA.
Reviewed by BENSON
on
August 23, 2017
Rating:
No comments