UFUGAJI BORA WA KAMBALE
Kambale
(Ietalurus Punetaus), ni aina ya samaki ambao wana majina mengi kulingana na
eneo na jamii husika. Samaki hawa unaweza kusikia wakitajwa kwa majina mengine
kama vile, kambale channel, koleo, samaki kidevu Na kuendelea.
Asili ya Kambale
Asili ya samaki hawa ni Amerika ya Kaskazini. Samaki hawa hukua
kwa haraka sana, na kuwa na uzito mkubwa. Aina hii ya samaki hupendwa na watu
wengi kwa kuwa nyama yake ina ladha nzuri na ni laini sana.
Samaki hawa huzaliana vizuri zaidi wanapokuwa mtoni au sehemu ambayo wanapata tope. Mfugaji anapokusudia kufuga aina hii ya samaki kibiashara, ni lazima kusakafia bwawa ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababishwa na samaki hawa.
Umbile lake
Samaki aina ya kambale wana umbo refu, pia ni wapana kuanzia
shingoni, ingawa kichwa ni kidogo, na upande wa mkia ni mwembamba. Samaki hawa
wana rangi ya kijivu na wengine nyeusi.
Jinsi ya kulisha kambale
Unaweza kulisha kambale kwa kutumia unga wa samaki, maharagwe
yaliyosagwa, mahindi, mchele pumba, ngano na bidhaa nyingine. Unaweza kujenga
mfumo ambao utawawezesha samaki hawa kupata aina mbalimbali za wadudu, pamoja
na majani, ili kusaidia wapate mlo kamili.
Ukuaji na uvunaji wa kambale
Aina hii ya samaki, wakitunzwa vizuri, wanaweza kukua kwa haraka
na kuwa na uzito mzuri unaoweza kumpatia mfugaji faida nzuri. Unaweza kuanza
kuvuna kambale baada ya miezi sita tangu walipopandikizwa kwenye bwawa.
Soko la kambale
Fikiria soko la samaki kabla ya kuanza kuzalisha.
Wafugaji walio wengi, wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa samaki kwa kufuata mkumbo bila kutambua kwanza soko watakalozalishia samaki hao. Jambo hili huwafanya wafugaji kuwa na kipato kidogo tofauti na nguvu waliyotumia kuzalisha.
Inapofikia wakati wa kuvuna samaki, kiasi kikubwa huuzwa papo hapo bila kufika kwenye soko halisi, jambo linalosababisha kipato kuwa duni. Ni vyema mfugaji akawa na soko maalumu ambalo atazalishia. Unaweza kuzalisha kwa ajili ya shule, hospitali, vyuo, au taasisi yoyote. Halikadhalika jamii inayokuzunguka na taasisi nyinginezo.

Mambo ya kuzingatia kabla
ya kufuga samaki
• Fahamu ni
aina gani ya samaki inayopendwa zaidi katika eneo ulipo.
• Samaki wanaopendwa wanatakiwa wawe na ukubwa gani.
• Kiasi cha samaki kinachohitajika katika soko ulipo.
• Ni kipindi gani ni kizuri kwa uvunaji wa samaki.
• Ni wakati gani mzuri wa kuuza samaki.
• Je, katika eneo lako kuna mfugaji mwingine anaezalisha samaki kwa ajili ya soko hilo?.
• Bei ya aina ya samaki unaozalisha ikoje?

Wasikilize wateja
Wakati wote
mfugaji anapouza samaki, ni lazima kusikiliza kwa umakini, wateja wako
wanasemaje.
• Je, wanapendelea samaki unaouza.
• Je, samaki wako ni wadogo sana au ni wakubwa sana.
• Wakija kununua wananunua kwa kiasi gani, kikubwa au kidogo.
• Je, wanapendelea uzalishe zaidi?
• Je, kuna wafanyabiashara wanataka uzalishe zaidi ili nao wanunue.
• Wanataka samaki wawe kwenye ubora gani.
• Wanaridhika na bei unayowauzia.

Fuata haya kwa ufanisi wa
soko la samaki
• Hakikisha
samaki wako katika hali ya usafi na vyombo salama unapovua tayari kwa kupeleka
sokoni.
• Samaki ni bidhaa inayoharibika kwa haraka, hivyo hakikisha unawapeleka sokoni mara tu baada ya kuwavua.
• Hakikisha gharama za usafiri, utunzaji na uhifadhi, zinalipwa kutokana na bei ya soko.
• Kumbuka gharama za uhifadhi wa bidhaa inayoharibika haraka kama samaki ni kubwa, hivyo vua kwa awamu kulingana na mahitaji.
• Unaweza kuongeza thamani ya samaki kwa kufanya mambo ya msingi yanayohitajika kwenye uandaaji wa samaki, kama vile kuparua na kutumbua.
• Unaweza kuwasafisha, na pia kuwakaanga kulingana na soko husika.
Kwa kuzingatia mambo hayo machache, mfugaji anaweza kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuwekeza kwenye mradi wa ufugaji wa samaki. Pia ni muhimu kuzingatia mahitaji muhimu ya ufugaji wa samaki, ili kuepuka gharama zisizo za lazima.

Tengeneza chakula cha samaki
mwenyewe
Mfugaji anaweza
kupunguza gaharama za kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza
chakula mwenyewe kwa kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia
resheni rahisi ambayo itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.
Mahitaji
• Pumba ya
mahindi sadolini 1.
• Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
• Dagaa sadolini 1.
• Kilo moja ya soya.
• Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.
• Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
• Dagaa sadolini 1.
• Kilo moja ya soya.
• Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.
Namna ya
kuandaa
• Changanya
malighafi hizo kwa pamoja.
• Saga hadi zilainike.
• Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
• Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
• Anika kwenye jua la wastani.
• Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
• Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.

Reviewed by BENSON
on
August 22, 2017
Rating:
No comments