KILIMO BORA CHA CHOROKO.
Choroko ni zao la chakula na biashara
lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium. Zao hili
likilimwa vizuri hutoa mavuno kati ya Kg 400 hadi 900 kwa ekari moja. Hivyo kwa
yeyote yule mwenye nia ya dhati ni vyema akajikita katika kuhakikisha analima
kilimo hiki.
UDONGO NA HALI YA HEWA IFAAYO.
Choroko hustawi katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji.Hulimwa
kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine
zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu.Hili ni zao linalostahimili ukame.
AINA ZA CHOROKO
Kuna aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi
mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani.
1. CHOROKO ZINAZOTAMBAA-hizi ni
choroko ambazo zinarefuka sana na hutambaa sehemu mbalimbali.
2. CHOROKO ZINAZOSIMAA-Hizi ni
choroko ambazo zinakuwa kwa kusima kwenda juu.Hizi huchukua muda mfupi kukomaa
wastani wa siku 60-70.
KIPINDI KIZURI CHA UPANDAJI WA CHOROKO
Choroko hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa
mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga.
NAFASI ZA UPANDAJI WA CHOROKO NA
KIASI CHA MBEGU
Choroko huitaji mbegu kiasi cha kilogram 8 hadi kumi kwa ekari moja.
Panda choroko zako kwa nafasi ya sentimeta 30 mastari na mstari na sentimeta 10
shina hadi shina (30 x10 )sentimeta au (40 x 8 )sentimeta.
SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI
Kama shmba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani
tano kwa ekari na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya NPK kg 50 kwa
ekari.weka mbolea zote kabla ya kupanda.
UMWAGILIAJI
Kama umepanda kipindi cha ukame sana au unalima kilimo cha umwagiliaji basi
mwagilia shamba lako upate unyevu wa kuotesha mbegu, kisha baada ya mbegu kuota
kaa siku 6 hadi 10 na umawgilie tena. Mara tatu za kumwagilia zinatosha kwa
choroko.
PALIZI
Palilia shamba lako mapema kuzuia magugu.Palizi moja inaweza kutosha.
MAGONJWA YA CHOROKO
1. Yellow mosaic virus ( Ugonjwa wa manjano)
Dalili: mmea unakuwa wa njano na madoa ya njano katika majani.
Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili magonjwa.
2. Powdery Mildew (Ukungu)
Dalili-Majani yanakuwa na vidoti vya njano ambavyo vinabadilika kuwa vya
kahawia au kijivu haraka na ambapo kunakuwa na unga unga katika majani.
Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili ukungu,Pulizia dawa za ukungu
(Fungicide).
anza kupuliza wiki tatu baada ya mimea kuota na kuendelea kulingana na hali
halisi.
3. LEAF SPOT (Vidoti katika majani)
Dalili-majani yanakuwa na vidoti vya mviringo na visivyo na umbo maalum ambapo
katikati yanakuwa na rangi rangi ya kijivu na weupe na mistari ya rangi
ya wekundu-kahawia au nyeusi-kahawia.ugonjwa huu husababisha hasara hadi ya
asilimia 58 ya mapato.
Kinga na Tiba-Panda mbegu inayostahimili ugonjwa huu,Choma mabaki ya mimea hii
na ile ya jamii moja baada ya kuvuna.Pulizia dawa za ukungu (Fungicide) Katika
nafasi ya wiki mbili mbili kama eneo hilom linashambuliwa mara kwa mara na
ukungu.
WADUDU.
Kuna wadudu mbalimbali wanaoshambulia choroko kama vile
aphidi,funza wa vitumba,nzi wa maharage.Wazui wadudu hawa kwa kupuliza dawa za
wadudu mara tu baada ya mimea kuota,dawa kama karate,twigathoate,dimethote na
nyinginezo zinaweza kutumika.
UVUNAJI
Mara tuu choroko zinapofikia asilimia 85 ya ukaukaji zinabidi zivunwe
ukichelewa zitapukutikia shambani.
KILIMO BORA CHA CHOROKO.
Reviewed by BENSON
on
August 16, 2017
Rating:
No comments