FAIDIKA KWA KULIMA KILIMO BORA CHA FIGIRI.
Ulimaji wa mbogamboga hususani figiri ni shughuli
nzuri ambayo hufanywa na baadhi ya watu wanao jikita katika kujipatia kipato.
sasa leo nami nimependa kukupa somo mpendwa wangu kuhusu hiki kilimo.
Naam kilimo cha mboga mboga kinawatoa watu katika hali ya
ukata na kuwapa maisha ya kati na hata wakati mwingine kuwapeleka katika
ukwasi. Namaanisha shughuli hii itakupatia kipato cha kukidhi haja za kimaisha
yako endapo utaamua kulima.
Tuangalie mambo muhimu katika kilimo
hiki.
KUANDA SHAMBA / BUSTANI
huwezi kulima pasipo kuanda shamba au bustani yako.
Namna ya kuanda shamba.
Lima shamba lako vizuri na kuondoa nyasi/ magugu yote yaliyoootea katika
shamba. Kisha katua vizuri shamba lako kwa lengo la kuulainisha udongo wa
shamba lako.
Baada ya hapo mwagia mbolea ya kutosha katika shamba lako
kisha mwagilia maji ya kutosha kutengeneza unyevunyevu wa kutosha.
KUMWAGA MBEGU
Mbegu humwagwa katika bustani kwa kurusha. Lakini mbegu
hizi kabla hazija mwagwa kwenye bustani lazima uchanganye na mchanga kwa lengo
la kupatia nafasi pindi utakapo mwaga mbegu na kupelekea figiri kuota kwa
mpangilio. Lakini pia ikumbukwe mbegu huota ndani ya siku 3. Tangu kumwagwa.
Utaendelea kumwagilia bustani yako kila baada ya siku 2. Kwa
udongo wa tifutifu. Na kila siku kwa udongo wenye aina ya kichanga kwani aina
hii ya udongo hu pitisha maji kwa urahisi na kukauka haraka.
Mboga hii huchukua siku 30. Kuwa tayari kwa kuuzwa na
wateja kwenda kula.
Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada, endelea kutembelea
blog ya kilimo bora.
FAIDIKA KWA KULIMA KILIMO BORA CHA FIGIRI.
Reviewed by BENSON
on
August 18, 2017
Rating:
No comments