KILIMO BORA CHA PILIPILI MTAMA/MANGA
Pilipili mtama au kwa jina lingine pilipili manga
ni kiungo muhimu sana katika mapishi. Radha yake ya muwasho ndio kitu hasa kinachotafutwa
katika vipunje vidogo vidogo vya zao hili. Pilipili manga husagwa ili kupata
ungaunga kabla ya kutumika ingawa pia inaweza kutumika bila kusagwa.
Jina la kitalaam ni Piper nigram na kwa kiingereza
ni black pepper. Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na
linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar. Ingawa pia inaweza kukubali
katika maeneo ya Kagera
Pilipili nyeusi na nyeupe zote
hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki na kwa mapishi mengine mbalimbali. Nchi
za magharibi zina matumizi makubwa ya viungo hivi. Aidha pilipili mtama nyeusi
ndiyo huzalishwa zaidi hapa nchini.
Namna ya uzalishaji wa pilipili manga.
1.
Hali ya hewa na udongo
Viungo vingi humea katika
maeneo yenye joto la wastani kati ya nyuzi joto 24-26 na huzalishwa maeneo ya mwambao.
Udongo wenye rutuba na unaopitisha maji na wenye uchachu wa kiasi cha pH 6.5.
Mahitaji ya mvua ni mililita 1500-2000 kwa mwaka.
2.
Uchaguzi wa mbegu
Uchaguzi huzingatia mambo
yafuatayo:-
a) Urefu wa pingili na ukubwa
wa majani
b) Ufupi wa pingili unaoambatana
na majani madogo.
Tofauti iko hadi kwenye umbile
la matunda. Majani ya mche mama sehemu kinapokatwa kipando huondolewa wiki
mbili kabla ya kukata. Vipando vyenye macho (nodes) 3-4 humika. Macho mawili huzikwa kwenye udongo na kipando
kiwekewe kivuli. Inashauriwa kuweka mbolea ya samadi wakati wa kupanda.
pilipili mtama |
3.
Nafasi ya upandaji
Nafasi ya kupanda ni mita 2-3
kati ya mmea na mmea endapo miche imepandwa na miti inayotakiwa kupogolewa mara
kwa mara.
4.
Mahitaji ya mbolea
Matumizi ya mbolea hapa
Tanzania si makubwa katika kilimo cha viungo. Ingawa kiasi cha kilo 0.4 cha
Urea, kilo 0.3 cha Superphosphate na kilo 0.3 cha Potash ya Muriate kinaweza
kutumika kwa miche mikubwa.
5.
Miti ya kusimikia miche
Miche hupandwa kwa kusimikiwa
nguzo ili ikue kwa kujizungusha kwenye miti kama mijenga ua, n.k. Mti huo wa
kusimikia nao pia hupaswa kupunguziwa majani ili kupunguza giza. Kila kabla ya
msimu miti hiyo hupaswa kupunguziwa matawi (pruning).
Kupogolea miche ya pilipili
mtama
Mche ukifikia miezi 18 inapaswa
kupogolea kwa kukata sehemu ya juu ya mche ili kufanya matawi mengine yachipue
chini ya mche. Inashauriwa mche kuwa na urefu wa mita 3-3.5.
Uvunaji
Maua ya kwanza hutoka baada ya
miaka miwili. Matunda hukomaa miezi tisa (9) hadi kumi (10). Uvunaji ni
mizunguko 5 hadi 6 kwa mwaka. Pilipili mtama inaweza kuvunwa kwa misimu miwili.
Mavuno ni kati ya tani 0.35 - 3.75 kwa hekta. Wakati wa uvunaji kishina cha
matunda ya kijani hukatwa kutoka kwenye mti kisha mbegu za huchambuliwa kutoka
kwenye vishina na kisha huanikwa juani kwa siku 3 hadi 4 ili kuhakikisha
zinakauka vizuri kabisa. Kiasi cha unyevu kiwe angalau 13 – 14%.
pipili mtama iliyovunwa. |
Kuhifadhi
Pilipili mtama iliyokaushwa
vizuri inaweza ikawekwa kwenye chombo kisichopitisha hewa na kudumu kwa miaka
hadi 20 bila kuharibika.
Masoko ya pipili mtama
Soko la pilipili matama
linapatikana ndani ya nchi na nje pia. Bei ya ndani ni kati ya Sh1,000-1,500.
Zao hili huuzwa katika nchi za Uganda, Kenya, Uingereza, Ujerumani, Mashariki
ya Kati, n.k. Bei ya Nje ni wastani wa dola za kimarekani 1,985 kwa tani.
(Tafadhali fanyia utafiti soko, data hizi ni za siku nyingi)
KILIMO BORA CHA PILIPILI MTAMA/MANGA
Reviewed by BENSON
on
July 09, 2017
Rating:
No comments