YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI YA MBEGU ZA MPUGA

Je umekuwa ukijihoji ni vipi utapata mbegu bora za mpunga? Kama jibu ni ndiyo basi makala haya yanakuhusu sana wewe kwani lengo letu ni kuona wewe unafanikiwa sana kataika kilimo.
Watu wengi wemekuwa hawafahamu ni mbegu ipi ambayo inafaa katika upandaji, na kosa hilo ambalo wanalifanya limekuwa likisababisha mazao nkupatikana kwa uchache zaidi, ila mukweli ni kwamba Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Hivo ili kuhakikisha unapata mazao mengi Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:

1. Mbegu za asili za mpunga
Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo. Kuna aina nyingi za mipunga ya asili inayolimwa sehemu mbalimbali hapa nchini kama Supa, Kahogo, Kula na Bwana, Shingo ya mwali, n.k. Wakulima wanazipenda mbegu hizi kutokana na kuwa na sifa kama vile ladha nzuri, uvumilivu wa matatizo mbalimbali ya kimazingira na kwa sababu ya uwezo wa mbegu hizi kustahimili katika hali mbaya ya hewa na hazihitaji uangalizi wa hali ya juu.

Sifa hizi ni matokeo ya mbegu hizi kumudu mazingira na uchaguzi wa mbegu uliofanywa na wakulima kwa miaka mingi. Hata hivyo, nyingi ya mbegu hizi zina uwezo mdogo wa kuzaa, zinachelewa kukomaa, ni ndefu na rahisi kuanguka.

2. Mbegu zilizoboreshwa:
Hizi ni zile zilizoboreshwa kutokana na mbegu za asili. Mfano wa mbegu zilizoboreshwa ni kama vile Katrin, IR54, na IR64. Zinazaa sana hasa kwa kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, hazikidhi ladha ya walaji na ukobolekaji wake si mzuri na baadhi hazistahimili kwenye mazingira mengi ya kawaida. Hii imezifanya mbegu hizi kukubalika na wakulima kwa kiwango kidogo sana.

Mbegu bora nyingine zilizozalishwa kutoka utafiti na kuonekana kupendwa kwa ajili ya mavuno mengi na ladha nzuri kama TXD88 na TXD85. Hivi karibuni imetolewa mbegu nyingine iitwayo TXD306 (SARO5), mbegu hii hupendwa na wakulima, wafanyabiashara na walaji kutokana na sifa yake ya mavuno mengi, punje ndefu kiasi na nzito, ladha nzuri na yenye kunukia pindi ipikwapo na kuliwa.



Hayo ndiyo makundi ya mbegu bora ya mpunga ambayo yatakusaidia kuweza kukua katika kilimo.
YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI YA MBEGU ZA MPUGA YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI YA MBEGU ZA MPUGA Reviewed by Muungwana Blog on May 26, 2017 Rating: 5

No comments