KILIMO BORA CHA PAMBA

Image result for kilimo cha pamba

Pamba ni moja la zao ambalo pia hurimwa nchini Tanzania, hukuzwa kwa kutumia tunda lake pia hilo tunda hua na nyewele nyeupe, hizo nywele ndio hutumika kutengeneza uzi na nguo. Pia mbegu za pamba hutumika kutengeza mafuta, mafuta ambayo tunatumia kupikia, namashudu ya mbegu hua na kasi cha protein ambayo mashudu hayo hutumika kama chakula kwa mifugo.


HALI YA HEWA NA UDONGO

Pamba hustawi vizuri katika maeneo yenye joto, kwa hapa tanzania hufanya vizuri katika mikoa ya kanda ya ziwa yaan chini ya 1400m kutoka usawa wa bahari mfano Mwanza, shinyanga na geita.
pamba huitaji kiasi cha mvua 25mm kwa miezi miwili ya kwanza,katika mwezi wa nne pamba huitaji kiasi cha mvua 75mm,na katika miezi inayo fuata pamba huitaji mvua ndogo ili kuwezesha pamba kukomaa, pamba hustawi vizuri katika udongo wa aina nyingi, japo kua haiitaji ardhi inayo tuamisha maji,ila katika udongo wenye PH chini ya 5.0 pamba haistawi vizuri.


AINA

Aina nyingi ambazo hulimwa Tanzania zimefanyiwa utafiti na kugunduliwa ukiriguru,aina nyigi za ukiliguru huitwa UK au UKA variety. mbegu hizo hufanya vizuri zaidi katika mikoa ya kanda za magharibi. aina nyingine zimetokea ilonga aina hizo nyingi huitwa IL mfano IL 85 Variety. mbegu hizo hufanya vizuri katika mikoa ya mashariki.



KUPANDA

Andaa shamba kwa kutumia jembe la mkono, ng'ombe au tractor, kama unapanda maeneo yenye udongo mzito weka matuta kwa kufanya mistari ya contua.

panda mbegu 6 hadi 10 katika kila shimo, nafasi hutegemea na eneo ulilopo. kama upo maeneo ya magharibi tumia nafasi 60cm x 15cm kama , kama unatumia matuta tumia nafasi 150cm na panda mistari miwili kila tuta. nafasi ya mistari ni 45cm na nafsi ya mimea ni 45cm

kama unapanda pamba katika mikoa ya pwani tumia 90cm x 30cm.



KUNG'OLEA

Mimea inapofikisha urefu wa 10cm hadi 15cm unatakiwa kung'olea, kwa maeneo ya magharibi acha mmea 2 katika shimo na kwa mikoa ya pani acha mmea 1 katika shimo.ng'olea mapema baada ya palizi ya kwanza.



PALIZI

Unatakiwa kupalilia pale unapo taka kung'olea baadae unaweza kupalilia kadri na jinsi magugu yanavo ota shambani.

katika mashamba makubwa unaweza kufanya palizi kwa kutumia viua gugu, kiuagugu kinacho fanya vizuri ni diuron, na zingatia kusoma maelezo ya mtengenezaji kabla ya kutumia.




MBOLEA

Kama mbolea ya samadi inapatikana unatakiwa kuweka mbolea mapema katika kipindi cha kuandaa shamba,

kama samadi haipatikani unaweza kuweka 125kg ya single super phosphate katika shamba la ukubwa wa hekta moja kama mbolea ya kupandia.

baada ya wiki 6 toka mda wa kupanda unaweka mbolea ya kukuzia yaani SA au CAN, tumia mbolea kiasi cha 125kg katika hecta moja ya shamba. nzingatia kuweka mbolea baada ya kupalilia na kung'olea.



 WADUDU NA MAGONJWA

 Pamba huasiliwa na wadudu wa aina nyingi sana mfano vitumba wa marekani, vitumba wekundu, vitumba wa awaridi, nematodes, mchwa na vidudu mafuta.

pia kunanjia mbalimbali ya kuzuia wadudu hao, njia mojawapo ni kama vile kutumia viuadudu , pulizia dawa angalau wiki mbili mara sita, pulizia dawa kuanzia wiki 6 toka kupanda.dawa za kuua wadudu ni kama carybryl na endosulfuan.



 Magonjwa yanayo asili pamba ni kama vile bacteria bright, fulsalium wilt na vertllium wilt.tumia dawa za fungus na pia zingatia kuanda mbegu zinazo staimili magonjwa.
KILIMO BORA CHA PAMBA KILIMO BORA  CHA PAMBA Reviewed by BENSON on May 28, 2018 Rating: 5

No comments